Ulizaliwa peke yako, utakufa peke yako. Tumia akili yako vizuri |
Siku
chache zilizopita niliandika mada ndogo yenye kichwa cha mada ‘KWANINI KUJAMIIANA NI HATARI KABLA YA NDOA.’Na
kuiweka kwenye magroup ya watsup,facebook na instagram (@eng.ngukiwamalekela)
ili kuona mitazamo ya watu hasa vijana juu ya hili. Kabla sijaeleza sarakasi za
huko nitaomba kurudia hapa kile kipande kidogo nilichoandika.
Kujamiiana hakuna nafasi yoyote
kuonesha mapenzi hata kama mpo katika mahusiano kwa muda mrefu au hata kama
ndoa ipo karibu sana na ni wachumba rasmi. Bali:
- Hupunguza mvuto wa msichana kwa mvulana
- Humfanya msichana awe mtumwa kwa mvulana
- Hofu ya mimba, magonjwa na kutojiamini
- Mwanaume kutooana umhimu wa kufunga ndoa na msichana huyu kwa maana anampa unyumba ambao ndio kiini cha ndoa, kama ni ugali hata kwa mama yake upo tu.
- Mgogoro wa nafsi na kukosa uhusiano na Mungu
- Mwanamke kuishi kwa kujihami (defensive) kwa kuhisi yeye ni (supplier) mtoa ngono tu bali mtu wa kuolewa ni mwingine.
- Kila baada ya ngono kwa mwanamke wimbo hubadilika kutoka ‘jitahidi tujitunze na tufikie malengo yetu ya ndoa’ na kuanza kuwa ‘ukinisaliti nitakuua wewe na kisichana chako au nitajiua, nimejitoa mwili wangu kwaajili yako, tafadhali nifichie aibu yangu’ huku mvulana yeye akijisifia kwa wenzake na kuwaeleza ulivyo mchakarikaji kumfurahisha kingono na unavyojibembeleza kwake ulivyo huna jeuri ya kumuacha.
- Nakukumbusha tu kwamba madhara ya ngono kabla ya ndoa yapo tu hata kama mtaoana lakini yapo na wahusika hujitahidi kuyapotezea hasa kisaikolojia, kiroho na kijamii.
- Labda niulize, hujawahi kuona mtu kapata sifuri kwenye mtihani wake wa mwisho, nabado utamsikia anasema ‘haijaniathiri kitu, na haya niliyapanga mwenyewe,watu kibao wamesoma lakini hawana lolote, nitatoka kivingine. Hivi ni kweli huyu mtu hajaumizwa na haya matokeo? Ukweli ni kwamba kaumia sana na hakuna namna ya kurudisha ule muda na rasilimali vilivyopotea, bali anajitahidi kupambana na dhamira yake kuuzima ukweli. Hata kwenye ngono ndivyo ilivyo.
Bora nusu shari kuliko shari kamili. Najua
ni ngumu kumeza hasa kama uliaminishwa kuwa huwezi, lakini chukua hatua na ugeuke.
Mwisho wa nilichopost.
Sasa pamoja na baadhi ya watu kuukubali ukweli japo unauma,
wapo waliosema yafuatayo ambayo niliyategemea na nilifurahi kwa maana walikuwa
wazi:
- Wapo waliosema hayo yalikuwa zamani sio kwa sasa
- Wengine wakawasemea na wenzao kuwa ‘wewe humu umejiandikia mwenyewe peke yako wengine hatukubaliani na hilo’
- Wengine wakasema ‘utaishije sasa bila kufanya ngono? Au unatakaa watu wafanye punyeto (masterbation)?
- Wengine wakasema ‘siku hizi wanaume wanataka kujaribu kwanza (kutest) ndipo waoe. Ukijifanya kubania utaishia hivyo bila kuolewa. (Japo mwenye huo mtazamo ndio huishia kuwa kisima cha majaribio na kuolewa ni kwa wengine)
- Wengine wakasema huwezi ishi katika mahusiano kama dada na kaka lazima mfanye tu.
- Na wengine wakaweka maneno ya kuamsha hashiki kwa wenzao ili waamini kabisa kuwa haiwezekani hata kidogo kumudu mhemko wa mwili pale utakapohitaji kufanya ngono
Nilichojifunza ni kwamba wengi wa waliokuwa wanapinga kabisa
ukweli huu wapo kundi la mwanafunzi niliyemtolea mfano kwenye post yangu hapo
juu. Watu kukubali kuwa ‘ndio nimewahi
kufanya lakini ni kwa makosa na iliniathiri na sitaki kurudia kosa au sitaki watoto
wangu waje kuishi hivi’ wanadhani ni ushamba na kujidhalilisha. Watu
wanapigia chapuo uongo ili tu ku draw tension ya wasio na msimamo.
Katika mada yangu sikulenga kuhukumu mtu ambaye amewahi
kukosea bila kujari mara ngapi, hapana. Mungu wetu ni Mungu wa kutoa nafasi ya
pili (second chance) kwa mtu aliyekosea. Naongea haya kwa maana wapo watu ambao
tendo moja la ngono lilizalisha mimba, magonjwa ya ajabu yasiyona tiba, aibu na
mvurugano mkubwa wa kifamilia na kuzalisha majuto ya daima.
Lakini wapo ambao
wamefanya mara nyingi nabado madhara yao pengine ni yandani zaidi na kwa nje
mtu hajayaona. Hii haimaanishi wamefanya aina mbili tofauti za ngono, hapana
bali ni Mungu tu anakuepushia na kukupa nafasi ya kubadilika akiamini kuna watu
fulani wanakutegemea hivyo akiruhusu pigo hilo wengi watapata shida sana kwa
kukosa huduma yako.
Mtu wa kundi hilo la pili ndiye kinara wa kupigia chapuo
utekaji wa dhamiri za watu kwa kujigamba kuwa hawezi kuishi bila ngono kana
kwamba anaviungo vya chuma ambavyo yuko makini kuweka oil na grease ili
visipate kutu. Kama lilivyojanga la UKIMWI ni rahisi sana kulitaja ukiwa huna
maambukizi. Hebu kutana na watu wanaoishi na maambukizi ya UKIMWI na uone
mtazamo wao, wanatamani kupona, wakiambiwa nenda eneo fulani uatapona
wanakwenda kwa gharama yoyote. Wakiambiwa ukila kitu fulani utapona, watakula
hata kama hakina radha.
Ndivyo ilivyo hata kwa wanaopigia chapuo ngono kwa kutumia
kondomu ni wale ambao hawana maambukizi. Kama huamini nenda kwa huyo
mfanyangono mwenzako mwambie ‘nimepima
na kugundulika na maambukizi ya UKIMWI, lakini nimekuja na kondomu kwahiyo tutafanya
ngono salama mpenzi wangu’, uone kama kuna sketi au suruali itashuka hapo,
ng’oooo hata busu tu atakukatalia na tumbo kuanza kumuunguruma.
Nikukumbushe tu kuwa UKIMWI upo Tanzania tangu 1983, ni zaid
ya miaka 33 iliyopita, na kizazi kinachojishughulisha sana na ngono ni vijana
ambao wapo chini ya miaka 30 au juu kidogo, hivyo wengi wanaishi na maambukizi
ya UKIMWI pengine kwa kuzaliwa nayo, hivyo unaweza kufanya ngono wote au mmoja
akawa hajawahi kabisa kufanya ngono na afya yake ni nzuri kumbe ana maambukizi
kutoka kwa wazazi wake na ni HIV carrier, hatumii ARV na CD4 zipo juu kama
kawaida.
Lakini pia mahusiano ni kipindi cha kuchunguzana, hivyo
mnaweza kwenda na badaye ukagundua tabia chafu ambayo haiwezi kuvumilika,
utafanyaje? Tuchukulie mfano mahusiano yamepamba moto na mnafanya ngono then
unagundua huyo mfanyangono mwenzako ni mshirikina aliyebobea na familia yao
kila mtoto wa kwanza huwa wanamtoa
sadaka kwenye mizimu na matambiko huko, nayeye ni kiranja wa hiyo kazi, wakati
huo mwanamke kashajazwa mimba, na mnasema tutaoana utafanyeje? Au unagundua
mwenzako ni jambazi la kutupwa, kuua kwake ni kama kunywa mtindi, utafanyeje?
Asilimia kubwa ya mahusiano yanayohusisha ngono huishia
kuoa/kuolewa na mtu ambaye humpendi kwa maana mvulana unaanza kumuonea huruma
mtoto atakayezaliwa baada ya kumpa mimba msichana hivyo unaamua tu kumchukua
kwa ushenga wa mtoto aliye tumboni. Hivyo upendo utakuwa kwa mtoto na sio mke napengine
kuwachukia wote. Msichana naye anaona aibu kuwa na mtoto ambaye atalelewa na
baba mwingine na hajuwi mtazamo wa watu kuona yuko vile napengine akaja kupata
mume ambaye hataki mtoto wa kumkuta, hivyo anaamua kumbana huyu aliyempa mimba
ili amuoe kwa lazima.
Umeyasikia mengi, suala la upande utakaofuata ni juu yako. Mungu amekupa dhamira ikusaidie kukuonya. Chukua hatua binafsi |
Katika wale waliokuwa wanacomment kuna mmoja aligusia suala
la punyeto au masturbation naomba nilifafanulie madhara yake hapa:
Punyeto/Masterbation ni tabia ya baadhi ya wanaume
kutumia mikono yao kusugua uume hadi kutoa mbegu za kiume na kujiridhisha
wenyewe (emotional/sexual self-satisfaction).
Madhara yake ni:
- Unavunja mishipa myembamba ambayo inasaidia resistance wakati wa haja ndogo, ule uthabiti wa uume kucontol mkojo unapungua hivyo ukienda kukojoa unakosa uwezo wa kuuzui hivyo utatoka kama bomba la maji hadi mwisho, na ukiendelea hadi ukubwani kwenye utu uzima basi mkojo ukikubana tu unajitokea wenyewe hapo ulipo kwa maana mawasiliano kati ya uume na kibofu yanakatika. Sasa kama utatembea na pampasi kama kichanga mimi sijuwi.
- Ikumbukwe hili linahusisha ubongo pia, na ukifika muda wa kuwa ndani ya ndoa utakuwa unatoa mbegu ambazo hazijakomaa (pre mature ejaculation), ambao ni ugumba kwa mwanaume.
- Mwanaume aliyezoea (addicted) kufanya punyeto hawezi kufurahia tendo la ndoa muda ukifika kwa maana joto linalotolewa na mkono ni kubwa kuliko linalotolewa na mwanamke, hivyo atamuacha mkewe na kuendelea na tabia yake.
- Wengine wanapata madhara hadi nje kwa kupata vidonda na makovu (physical wounds and scars ).
UTAACHAJE
Kwanza kubali kuwa ulichokuwa unafanya kina madhara makubwa
sana na ni hatari sana hivyo anza taratibu kupunguza na baadaye utaacha kabisa.
Pata matibabu kama ulipata vidonda na waone washauri nasaha ili kuata counseling
itakayokuimarisha ubongo wako na uanze safari mpya.
JE WASICHANA NAO
WANAFANYA PUNYETO?
Ndio. Katika semina ambazo tumekuwa tukifanya na vijana mara
nyingi hili limeibuka. Wapo baadhi ya wasichana kwa kuyaona mitandaoni au
kudanganywa na watu wamekuwa wakitumia vifaa vyenye muundo wa uume ili kufanya
ngono wenyewe kama ndizi, test tubes, tango, karoti nakadharika.
Madhara ya
vyote hivyo ni:
- Kusababisha michubuko katika via vya uzazi ambapo hupelekea makovu ambayo yanaweza kuziba mirija ya uzazi au kusababisha kuota virusi vitakavyopelekea uambukizo wa kansa ya shingo ya kizazi (cervical cancer)
- Kuwafukuza bacteria wazuri ambao wapo kwenye via vya uzazi kupambana na shambulio lolote la mangojwa fulani. Ikumbukwe kutokana na mifumo yetu ya uzazi kwa mwanaume hali ya ugonjwa fulani wa ngono dalili zikianza kuonekana nje, huenda ndani bado hali sio mbaya sana, lakini kwa mwanamke hali ikianza kuonekana nje ndani ujue hali ni tete zaidi.
- Lakini pia vitu vyote hivyo vinaweza kukatikia na kubakia ndani, utavitoaje?
KWA WAVULANA NA
WASICHANA:Aina zote
za punyeto ni hatari, ushamba na ulimbukeni, acha kujaribujaribu kila
usikiacho.
Natamani nieleweke lengo langu kuandika haya sio kuhukumu au
kuonesha kuwa mtu aliyewahi kukosea ndio hafai, hapana. Lengo langu ni moja tu,
kama mimi na wewe hatujawahi kukosea basi TUMSHUKURU
MUNGU NA TUSIJARIBU KUKOSEA, TUITAWALE MIILI YETU NA KUPAMBANA NA VISHAWISHI
HADI NDOA. Kama mimi na wewe tumewahi kukosea lakini Mungu katuacha hai,
basi TUGEUKE NA TUSIRUDIE KOSA, TUTUMIE
VYEMA NAFASI YA PILI TULIYOPEWA NA MUNGU ILI KUHAKIKISHA ANGALAU TUNAKUJA KUWA
NA KITU CHA KUWAASHAURI WATOTO WETU. Ukigeuka Mungu anapunguza madhara (Spiritual and mental rejuvenation), utakuwa na amani na mfumo wa utendaji kazi wa nafsi yako unarekebika na kuwa mzuri, na Baraka za Mungu utaziona kwa macho yako.
‘Kama wewe unatabia
fulani, basi usitudanganye kwamba wote wanatabia au mtazamo kama wako.
Ulizaliwa peke yako na utakufa peke yako. Wote tutakufa, ishu ni nani kafa
kivipi. Mungu ametuumbia dhamiri inayotuonya na kutukumbusha kugeuka, usikubali
mtu aiteke dhamiri yako na kukuburuza na mtazamo wake hasi ambao hujuwi
utakupekeka wapi. Uking’ang’ana na njia ya POTELEA MBALI, utatokea mtaa wa
NINGEJUA’
Eng Nguki Herman. M