Mungu yuko upande wetu. Tujibidiishe kusali na kufanya kazi. |
Tumsifu
Yesu Kristu.
Namshukuru Mungu paoja nanyi kwa neema ambazo
anatujalia kila siku ingawa hatustahili. Maovu yetu mara kadhaa yametutenga
mbali na Mungu na kutusogeza kubaya ambako haukuwa mpango wa Mungu Zaburi 103:12 Kama mashariki ilivyo mbali na
magharibi, Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi
Ni kweli, tumefanya maovu na lazima tukiri wazi kwa vinywa
vyetu
Zaburi
106:6 Tumetenda dhambi pamoja na baba zetu,
Tumetenda maovu, tumefanya ubaya.
Isaiah
59:12 Maana makosa yetu yamezidi kuwa mengi mbele
zako, na dhambi zetu zashuhudia juu yetu; maana makosa yetu tunayo pamoja nasi,
na maovu yetu tumeyajua;
Jeremiah
14:20 Ee Bwana, tunakiri uovu wetu, na ubaya wa
baba zetu; maana tumekutenda dhambi..
Mara
nyingi nikiwa nasoma chuoni, wakija wanafunzi ambao walishamaliza walikuwa
wanatutia moyo kwa kutuambia shule sio ngumu mtafaulu tu. Ni
kweli nen hili ni muhimu na la faraja kwa wanafunzi wanaoendelea. Mimi pia
nimemaliza hapa chuoni, lakini niwaambie tu bila kuumauma maneno, shule ni
ngumu, ten asana tu Ndio shule sio rahisi hata kidogo. Kwa sentensi hii sina
maana kwamba huwezi kumaliza au kufaulu vizuri, bali juhudi za makusudi na
kujitoa sadaka ya muda lazima viwepo kwa nguvu zote.
NINI
KINAFANYA CHUO/SHULE WAKATI FULANI KUWA NGUMU KUPITA KAWAIDA
Kwa
ambao wamewahi kutumia computer:, ikitokea unahamisha vitu vingi kutoka kwenye flash disk kwenda kwenye
computer au kinyume chake, utaona computer inaandika two days left ,
ikimaanisha hiyo kazi ya kuhamisha mafaili yako itachukua siku mbili, baada ya
dakika kama tatu, utaona inakambia bado siku moja, baada tena ya dakika chache
inakuambia bado msaa sita, tena baada ya muda mfupi inakwambia bado nakika
kadhaa, badaye sekunde na ile kazi inakwisha ndani ya robo saa tuamaa na kuongeza juhudi hifanya
iishe mapema na kwa ufanisi. Hivyo kama mtu sio mvumilivu na anasafari baada ya
lisaa limoja, akiona ile 2 days left, basi anaahirisha na kuona itamchelewesha.
.Kwa tafsiri rahisi ni wamba kazi yoyote mwanzo huonekana kubwa na nzito sana ,
na ndiyo ilivyo, lakini kutokata Zipo
sababu nyingi sana. Pamoja na changamoto ya uwezo binafsi wa mwanafunzi
kitaaluma, ulevi, msongo wa mawazo na majukumu yanaayozidi uwezo, naomba
nizitaje sababu kongwe mbili ambazo ni UVIVU
NA NGONO.
UVIVU: Mithali 19:15 Uvivu humtia mtu katika
usingizi mzito; Na nafsi yake mvivu itaona njaa.
Sina sababu ya kuanza kudadavua uvivu ni nini. Kwa kifupi
ni hali ya mtu kukwea kutimiza wajibu wake kwa makusudi. Mvivu hufurahia
matokeo mazuri pasi na kuangalia mchakato ulioleta matokeo hayo. Uvivu upo
kwenye vitu vingi sana. Huenda ni katika kusoma, au katika kusali. Mtu mvivu
kusali hupima nguvu za Mungu kwa vitu vichache alivyovichagua yeye. Kwa mfano
akiwa hahudhurii jumuiya, bali misa anaenda na mambo yake ynamuendea vizuri,
basi anaridhika na kujiambia kuwa Mungu katosheka na donoadonoa yake kwenye
mikusanyiko ya sala, hivyo wale ammbao wanaenda jumuiya na kufanya kazi kadha
wa kadha za kanisa, nabado mambo yao ni magumu, anadhani hawapo sawa kiimani au
wanakosea mahala fulani.
Wito wangu kwenu ni kusali misa na sala za jumiya kila
siku kwa maana hujuwi lini litazungumzwa lipi ambalo litakufaa wewe wapi hasa
baada ya maisha ya shule. Epuka kufanya substitution ya muda wa Mungu na vitu vingine kama chakula, stress
nakadhalika.
Mifano yenye undugu na
uvivu hatari:
- Kama ni muda wa kuanza kipindi cha dini, na wewe ndio upo kwenye foleni ya chakula na roho haikuumi kabisa, ujue kuna changamoto.
- Kama akikukwaza mtu fulani hasa yule ambaye unadhani ndio muhimu kuliko kitu chochote, basi unafunga vyote including mambo ya Mungu, except chakula tu, ujue kuna changamoto.
- Kama uko addicted na kitu fulani mbacho ndio starehe yako eg mpira, movie etc na kama ndio unatazama muda wa kipindi cha dini na kuona bora uendelee kutazama, ujue kuna shida somewhere.
- Hata kama umetoka kipindi cha mwisho darasani saa 1:20 au hata saa 1:30 jioni na kuna nafsi inakuambia ‘umechelewa sana, dakika 15 hazitoshi kwenda hadi dini, bora tu utembee taratibu, ukale upumzike’ , hiyo faraja siyo ya Kimungu.
- Au ukisikia wimbo wa Roho Mtakatifu unaimbwa, basi unajiambia ‘nimeshachelewa, hakuna sababu ya kwenda sahizi, nitaenda tu kesho’ hapo ni tatizo, ni uvivu huo.
- Mtu mvivu anateemea mijiza tu bila imani na mapendo, anawaza habari za kuambiwa ;POKEA MUUJIZA WAKO, WALE KUKU WAKO WATAANZA KUZALIANA KWA FUJO HADI BANDA LISITOSHE, Unajibu Aminaaaaa , wakati kuku wenyewe unawapa chakula mara moja kwa wiki, kila siku wanaumwa new castle . Hapo hata akisema KUKU WAKO WATAANZA KUTAGA MAYAI MATATU KWA SIKU ,’ Na wewe unajibu Aminaaaa. Huo ni uvivu wa kufikilia.
- Ref, : Baba na mama walikuwa na ugomvi kwenye familia, na wakaenda kwa mtu anajiita nabii na mtumishi wa Mungu. Lengo wapokee muujiza wao wa shetani anayesumbua familia yao. Jamaa akawaambia kuwa Roho wa Bwana anamshuhudia kuwa mama ni mshirikina, kumbe mama hata hana lolote masikini,familia ikaanza kuvurugika hadi walipoenda kwa padre kusuluhisha. Tena baba ni msomi mweye PhD , nikawa najiuliza hii sio academic PhD, labda ni PH ya soil inayokaribia acidity. Yote haya ni matokeo ya uvivu wa kufikilia na kutaka matokeo ambayo hujayatolea jasho kutafuta.
Tufunguemioyo yetu na kumtukuza Mungu kwa kazi zetu na vipawa alivyotujalia Mungu wetu |
NGONO: Ni kujamiana nje ya utaratibu (kabla
na nje ya ndoa). Kujamiiana ndani ya ndoa huitwa TENDO LA NDOA. Ni takatifu,
halali na linatamkika kirahisi. Pia matokeo yake ni furaha kwa kila mtu, lakini
matokeo ya ngono hayapokeleki hata kama mtu ni tajiri na ana kila kitu.
Katika mazingira ya chuo, mihemko ya kuhusiana
kwa pupa ni major consumer wa kuwapoteza utashi watu. (Watched
Hot Friday Movie)
Ninapozungumzia
ngono ninalenga michakato yote yennye mlengo huo na mawakala wake. Mifano:
·
Mara
ngapi umevaa mavazi ya makwazo na kuwavuta watu kingono. Kwa maana mwingine
unaweza kumuamsha hashiki mtu na akaona wwewe hauingiliki, hivyo anagain momentum
ya kwenda kumshawishi mwingine aweze kutimiza uovu wake huo.
·
Mara
ngapi umekuwa kinara wa kuahidi tu watu kwamba utaolewa/kuwoa? O level, A
level, JKT, wiki la registration, unayesali naye, classmate, mnayesoma naye
elective course, halafu unaota eti hawana effect, subiri tu utaelewa siku moja.
·
Mwanafunzi
wa mwaka wa kwanza kabla hata test one hujafanya, hiyo UE ndio hata hujui
inafananaje, but tayari umesema kuna mtu yupo hoi hajiwezi juu yako. Hapo
inatoa picha ya moja kwa moja what is your primary goal. Sijasema kwamba
mahusiano mabaya, hapaa, lakini yanahitaji kujipanga, utulivu wa nafsi na mwili
yaliyopita kwenye MVUTO, MAWASILIANO na
baadaye MAHUSIANO.
·
Mara
ngapi umejithaminisha sura yako na kujiona wewe ni bora sana hivyo hakuna
atakayekupa shida kwenye mahusiano kutokana na uzuri wako hasa kwa wasichana (kioo hakidanganyi). Lakini ukweli ni kwamba
wewe huwajui wanaume, bali unawajua wavulana tu. The sme kwa wavulana, mostly
tunawajua wasichana ambao bado wako kwenye makuzi, na tunajidanganya kuwa ni
wanawake.
·
Msichana,
once you put your skirt off, everything is off. Ni rahisi sana, mtu akikuona na
utulivu ukampotea , akija anaongea hadi anatetemeka , msichana na wewe ndio
unaona unamkomeshaaaaa kwa uzuri wako kumbe mwenzako pale akili zake za kawaida
hazipo, in such akianza kukusogolea towards your direction, huruma inakuingia,
akisema mguu pande, unajibu mguu sawa. Baada ya kukufahamu, Yeye mweyewe tena
anakuambia, nyuma geuka, mbele tembea, Kiruuuuuu, unaanza kulalamika mbona
harudi, kwani aliona nini that day? Jibu ni kwamba hakuona kitu, coz angekiona
kitu angekirudia tena kwa mara nyingine..
JE
TUSIINGIE KATIKA MAHUSIANO?
Tuingie tu, lakini
uwe kweli ni muda sahihi, mmejiandaa vya kutosha na uhakika wa kupropagate, hii
inahusisha mtazamo wa kiimani na kirasilimali. Kumbuka hii ni tofauti na
urafiki, kwa maana urafiki hautafutwi na hauna limitation, bali mahusiano
hutafutwa na yana limitation. Lakini pia jifunze kuweka mahusiano bila ngono.
Tawala mwili wako, vaa mavazi ya staha, jikubali kuwa wewe ni binadamu uliye
kamili.
Katika mazingira
fulani roomates wana attribute watu tuingie kwenye mahusiano kutokana na huduma
ambazo wanazipata kwa hao wanaowaita wapenzi wao, wakati sio wapenzi bali ni
wafanya ngono wenzao, eg wakiugua etc. Au simu zao wakiongea na kubembelezana
usiku, masikinini wewe tumbo linakuunguruma na kuona kama Mungu kakusahau. Hivi
umekosa vipimo vya kupma kazi za Mungu?
KAMA ANALAZIMISHA
NGONO, NITAKATAAJE WAKATI NAMPENDA?
Sio kweli, huo ni
unafiki. Upendo hauunganishwi na ngono, kuna kitu kimukuscorpion na unajifanya
huoni huo uchfu na shimo ambalo mnajichimbia wote wawili hasa msichana.
- · Kwanza mwambie wewe sio chombo cha starehe, hivyo mkataba wa ngono unauvunja rasmi.
- · Akiendelea kulazimisha mwambie haupo tayari kuendelea na hayo mahusiano.
- · Punguza mawasiliano na badaye acha kabisa.
- · Utaumia kidogo kwa kipindi cha mwanzo na baada ya muda fulani utagain momentum ya amani. Bora maumivu kidogo ya sasa kuliko maumivu ya kudumu badaye.
- · Usikubali tena kukutana naye sehemu za faragha , anaweza kukudhuru kwa namna yoyote endapo utakataa kutimiza matakwa yake. Mkikutana msalimie kama kaka/dada.
- · Acha kukurupukia mahusiano mapya mapema, tuliza kichwa fanya mambo ya msingi sana hasa sala na shule.
VIPI
JUU YA UHAKIKA WA MTARAJIWA WANGU KUWA ANAJITUNZA HUKO ALIKO?
Haikuhusu. Wewe heshimu
mwili wako, wekeza kwenye sala, Mungu atakulindia huyo ambaye humjuwi, kwa
maana kujiliinda kwako ni sala pia. Once ukimpata mkakati wa kwanza wa kuuweka
ni kuweka mkataba kuwa NGONO NI ADUI WA
MAHUSIANO . Na utamjua siku ya ndoa,
na ukisema basi wewe unaanza taratibu majaribio ya mwili wako kisa una
uhakika utamkuta used, basi wewe hautofautiani na wapiga lamli ambao wapo very
detailed kuongea mambo ambayo hawawezi kuprove. Hii ni kwasabau hata mchumba
wako aliyekutolea posa na mahari anaweza kufa siku moja kabla ya ndoa, na
asikuoe, wala hawawezi kusema marehemu kaacha mjane mmoja ambaye alitakiwa
kumuoa kesho.
Kwa
hayo machache niwatakie kila la heri katika masomo yenu, na Mungu awasaidie
sana, nasi tunawaombea san ili mpate wepesi katika masomo yenu. KARIBUNI KWENYE
MAHAFALI KESHOKUTWA 25/11. Tumsifu Yesu Kristo. ( 23/11/2016- TMCS SUA NEW HOSTELS)
Eng Herman Nguki wa
Malekela (Bsc Irrigation & Water Resources Engineering 2012-16- SUA)
Email ngukiherman@ymail.com instagram:@eng.ngukiwamalekela
Tembelea www.ngukiherman.blogspot.com mara kwa mara kujisomea mada mbali mbali za vijana, mahusiano na kanisa. Karibu ujifunze.