I am targeted to change youth's mind set towards positivity.

I am targeted to change youth's mind set towards positivity.
I am targeted to change youth's mind set towards positivity

Wednesday 2 November 2016

Nampataje Mchumba Mwema?-Dr Godbless Nicetus Massawe

Mshirikishe Mungu katika kuanza mipago ya kuingia  kwenye mahusiano, utafurahi daima

SEMINA: KANUNI SABA ZA KUMTAMBUA MCHUMBA ANAYETOKA KWA MUNGU

MAANA YA MCHUMBA
Mchumba ni mvulana au msichana ambaye ameweka ahadi ya kuoa au kuolewa baada ya kipindi Fulani.Ili uchumba uwepo lazima yawepo makubaliano baina ya watu wawili mvulana na msichana

HATUA ZA UCHUMBA
Ili uchumba utambulike rasmi ni unatakiwa kupitia hatua zifuatazo:-

(A)URAFIKI
Urafiki si uchumba bali unaweza kuzaa uchumba wapo waliokuwa marafiki baada ya kutakiana uchumba na wapo walokuwa marafiki wa kawaida lakini baadaye wakaamua kuwa wachumba.ni kawaida mtu kuwa na marafiki wengi lakini mchumba ni mmja tu sifa za mchumba ni tofauti sana na sifa za rafiki Marafiki wa jinsia tofauti ni lazima wajue nini kusudi la urafiki wao mfano wa makusudi ya urafiki ni
 BIASHARA
 MASOMO
 MAOMBI

(B)TAARIFA KWA WAZAZI
Hii ni hatua ya pili ana ya juu sana katika marafiki wa uchumba kumbuka kuwa marafiki wa uchumba si wachumba mpaka hapo taratibu zote zitakapokamilika .Ni hatari sana kuwapa taaarifa wazazi bila ya kuwa na hakika ya kuoana au kabla ya kufanya uchunguzi wa kutosha kuwa huyu ndiye chaguo sahihi toka kwa Mungu.kiafrika ukimchagua mtu umechagua familia na ukoo wake na kabila pia kuna ndoa nyingi zimevunjika kwa sababu watu walimpenda mtu na si familia na ukoo pia .kiafrika ukoo unaweza kukataa au kumkubali mtu hivyo mwombe Mungu kwani hakuna linaloshindikana kwake.Baada ya wazazi kukubaliana ndipo taratibu nyingine hutolewa kama mahari hapa uchumba huanza kuhusisha familia mbili na kuingia kwenye uchumba

(C)MAHARI
Ni kitu au vitu ambavyo wazazi wamekubaliana kitolewe kwaajili ya binti yao japo kuna makabila ambayo mahari hutolewa na mwanamke hayo ni makubaliano tu na ni taratibu za watu ambazo ni nzuri kadiri yao.Mahari ni jambo la kibiblia Mw 29:18-26 hivyo haina sabab ya kuipinga bali utu wa mtu utazamwe .Baada ya mahari uchumba hukamilika na ndipo pete ya uchumba huvalishwa,yafuatayo ni maneno ya kusema wakati wa kuvishana pete ya uchumba
”FULANI……..NAKUVISHA PETE HII KUONESHA NA KUTANGAZA HADHARANI KWAMBA NAKUPENDA,TENA NAKUAHIDI KUWA UTAKUWA MKE WANGU WA MAISHA SIKU ZA KARIBUNI,KILA UNAPOIONA PETE HII UKUMBUKE AHADI YETU,BWANA YESU TUNAKUOMBA UTUSAIDIE TUWE WAAMINIFU.”

TOFAUTI YA MAHARI NA POSA
Mahari ni kitu au vitu ambavyo hutolewa na mwanamme kwa wazazi wa mwanamke kwa makubaliano ya kuoana watoto wao, hii hutolewa mbele ya mashahidi wa familia zote mbili ,mahari si lazima iwe pesa inategemeana na makubaliano ya wazazi.Kwa wakristo kuweni makini kwa maana kuna baadhi ya taratibu za mahari huambatana na ibada kwa mizimu hii ni hatari kwa mstakabali wa wanandoa watarajiwa,
POSA hii huitwa pia kishika uchumba hiki ni kitu chochote kinachotolewa na kijana anayetaka kuoa kwenda kwa wazazi wa msichana chenye thamani yoyote.Posa haina majadiliano yaweza kuwa kukuk,mbuzi ,njiwa nk,kwa baadhi ya makabila wanapotaka kuoa hupeleka barua kwa wazazi wa mwanamke na kueleza nia yao ya kutaka kuoa na kuweka kiasi Fulani cha pesa barua hiyo husomwa kisha binti huulizwa kama anajua lolote juu ya kijana huyo anapokubali ndipo utarartibu wa kupanga mahari hufanyika.Baada ya uchumba kuvunjika mahari inaweza kurudi kutegemeana na kabila na makubaliano lakini posa hairudi
(D)KUTANGAZA KANISANI
Baada ya makubalian ya wazazi watoto waoane wachumba watakwenda kwa uongozi wa kanisa kuwaeleza japo ni vema kuwashirikisha viongozi wa kiroho mapema zaidi kabla hata ya mahari. Ushauri kutoka kwa watu wafuatao ni muhimu kwa wachumba kabla ya kuoana
 Mtu aliyekomaa katika maisha ya kiroho ,aliyetulia katika Roho mt
 Mtu asiye mmbea
 Mtu aliyedumu katika ndoa sio chini ya miaka 5-10 mwenye uzoefu ktk familia
 Awe katika familia isiyo na migogoro
Ni vema wakati wa kutangaza kanisani taratibu zote ziwe zimekamilika hata tarehe yaa ndoa

UMRI WA KUPATA MCHUMBA
Hili ni jambolinalowatatiza wengi hata wengine hujikuta wakichukua uamuzi usio sahihi kwa kudhani wanachelewa kuoa au kuolewa,. Mara nyingine wazazi marafiki na ndugu wamekuwa wakiwatia pressure vijana wkisema utaoa lini wewe? Kumbuka hatuongozwi kwa msukumo bali ROHO MT Yoh16:13; Rum 8:14 MH 3:1
Kiafya umri mzuri kwa msichana kuolewa ni miaka 20-30 umri huu msichana atajifungua pasi na hatari kubwa za uzazi umri mkubwa una matatizo mengi ya uzazi
Kwa upande wa wanaume miaka 25-40 kwa sababu katika umri huu kijana anaweza kutimiza majukumu yake kama baba
Pamoja na hayo yote umri sahii ni pale majira ya Bwana yanapotimia Is 49:8.watu wasikutishe waambie majira ya bwana hayajatimia.

KANUNI ZA KUMTAMBUA MCHUMBA ALIYETOKA KWA BWANA NA AMBAYE SIYE
Tangu mwanzo Adamu hakutafuta mke bali Mungu ndiye aliyemtafutia Mw 2:21-23 Biblia inasema mke mwema mtu hupewa na Bwana Haisemi mtu akatafute maana anayemwandalia mtu mke au mume ni Mungu na sio watu Mith 19:14
Hata hivyo suala la kufahamu huyu anatoka kwa Bwana ni kitendawili maaana vijana wengi tunaangaika sana Mungu hawezi kutuachia mtihani ambao tutafeli ila ni kwa kutojua tu kanuni tumejikuta tunaangukia kwenye mitego mibaya na kujutia maisha ya ndoa .Na wengine wapo kwenye uchumba huku wakiwa na wasiwasi kama huyo aliye naye ndiye au la .

Zifuatazo ni kanuni zitakazo kusaidia:-

(1)TAFUTA KWANZA UFALME WA MUNGU NA SIO MKE AU MUME
MT 6:33 Mungu anasema tuutafute kwanza ufalme wake na maengine yote akiwamo mke au mume tutapewa kwa ziada ,ndani ya ufalme wa Mungu ndipo kuna mke na mume bora MITH 19:14 ufalme wa mungu unapatikana kwa sala na maombi kwa kuambatana na matendo mema yaani kutimiza mapenzi ya Mungu. Mungu alipoona utendaji wa Adamu aliridhika akasema”Si vema mtu huyu awe peke yake ” Mw 2:18 ADAMU HAKUSEMA SI VEMA NIKAE PEKEYANGU. Dhambi zinatutenga na uso wa MUNGU NA TUKIWA KATIKA DHAMBI HATUPO KATIKA UFALME WA MUNGU ,Mke au mume mwema hapatikani nje ya ufalme wa Mungu IS 59:1-2 Jiulize kwa siku unasali mara ngapi unaomba mara ngapi kasha utajua unautafuta ufalme wa Mungu au la.

(2)UWE NA MACHO YA ROHONI
Mungu ni ROHO Yoh 4:24 hivyo huonekana kwa macho ya roho, kutumia macho ya roho ni kuangalia Mungu anasema nini na kutofuata watu wanasema nini.Kwa Mungu hakuna neon lisilowezekana Luk1:37. Tusiangalie mambo katika mtizamo wa kidunia mf Sara alitazama kidunia ndio maana hakuamini MUNGU ALIPOSEMA ATAPATA MTOTO Mw 18:6-12 .Zakariia hali kadhalika Luk 1:8-25 Hakika kwa Mungu yote yanawekana MT 7:7-9

(3)UJUE SAUTI YA MUNGU
Manabii na makuhani waliweza kusikia sauti ya Mungu Kut3:1-10,Yer 3:6,11 .mtume Paulo katika Mdo16:17 anakatazwa na Roho mt je alijuaje? Samueli pia alipata shida kujua sauti ya Mungu 1Sam 3:1-10 Ili ujue sauti ya Mungu ni lazima rohoni mwako lijae neno la MUNGU, ukikaa ndani ya Mungu na maneno ya Mungu yakikaa ndani yako omba chochote nawe utakipata Yoh15:7 Mungu anapotaka kusema na mtu anasema na roho yake, neno la Mungu ndani yetu ndilo litakalotuwezesha kusikia sauti yake.Zifuatazo ni njia ambazo Mungu hutumia kufikisha ujumbe kwa watumishi wake:-
 NENO LAKE
 MAONO
 NDOTO
 MAFUNUO
 WAJUMBE
 MAWAZO YAKO
 SAUTI NK
Tahadhari hata shetani au nafsi hutumia njia hizo pia,ili kujua hilo unapaswa kuwa mtu wa maombi na sala mara nyingi na kujitahidi kuishi maisha matakatifu.ili usikie sauti ya Mungu unapaswa uwe katika roho.Vijana wengi wameumizana na kuleteana madhara kwa maana walisikiliza nafsi zao wakidhani ni sauti ya Mungu
Ukiingia katika mahusiano kichwakichwa, kwa jeuri ya pesa au uzuri wako wa nje, utaelewa  vizuri kwanini Simba na Yanga wanaombeana njaa kila kukicha. Utajuta.


(4)ZIJUE SHERIA ZA NAFSI
Mungu alimuumba mtu katika utatu usiogawanyika akiwa hai yaani mwili,roho na nafsi MW1:26-27 Mungu aliumba roho maana MUNGU ni Roho ,MW1:1,Yoh4:24.mwili uliumbwa katika MW2:7 na pumzi ya MUNGU IKAMFANYA MTU NAFSI HAI MW 2:7B Nafsi ina nguvu sana na mara nyingi tunaongozwa na nafsi tukidhani ni Mungu Vijana wengi huongozwa na nafsi wakati wa uchumba wakidhani ni MUNGU.Mungu anaposema na watu husema na roho zao na sio nafsi RUM8:16 .

ZIFUATAZO NI SHERIA ZA NAFSI:-

SHERIA YA KWANZA
KILA KITU KIZURI NAFSI INA TAKA KUKIMILIKI
(Mf wa noti mbili za 5000/=)Yesu anasema ukitaka kumfuata ikane nafsi yako Mt16:24 kumpenda mtu mara nyingine si kibali cha kuoana wala si kwamba utamjua mchumba kwa kumpenda tu.Kumbuka hata wasiomjua MUNGU wanapendana kwa sababu wana nafsi.Upendo wa kweli ni lazima uletwe na ROHO MT GAL5:22.Nafsi nayo inapenda hivyo mchumba anayetoka kwa BWANA ni Zaidi ya kumpenda.

SHERIA YA PILI
NAFSI HUTOA MAFUNUO
Biblia inasema yamtokayo mtu ndiyo yanaujaza moyo wake hii ni sawa na kusema kuwa yamtokayo mtu ndiyo yaliyoijaza nafsi yake .Mf umegombana na mtu mchana usiku ukiwa peke yako umelala ugomvi unajirudia na unaweza kuona yule mtu anakuja na mnagombana tena.Nafsi ina tabia ya kudaka na kuhifadhi na kisha kutoa hivyo kama mtu anasikia mambo mabaya nafsi yake itayahifadhi na baadaye kuyatoa ,linganisha watoto wanaotoka katika familia zinazosali na wale wanaotoka katika familia zenye magomvi.Hali kadhalika kwa vijana unapomuona msichana au mvulana halafu ukampenda unapokuwa nyumbani nafsi yako inakuletea mtu huyo ili ajadiliwe na akili pamoja na mwili ,mjadala unaanza huyu anafaa sababu ni msomi kama mimi ,kabila langu,ni mzuri mpole nk.wakati huo pia mwili unakuwa mdau mkubwa akili na nafsi zinamwonesha mwili alivyo na maumbile mazuri ghafla mwili unaanza kudai haki yake hapo ndipo kijana anasema nimeona maono.Hayo ni maoni ya nafsi na si maono ya Roho mt.Ili kuyashinda hayo neon la Mungu lazima likae kwa wingi ndani yako KOL3:16.Mwili na nafsi vikiungana kumpenda mtu huwa ni hatari sana katika maisha ya kiroho mtu mtu haombi tena hasali na huondoa hofu ya Mungu na ni muda wa hatari mtu huanguka kiroho.Ukiona umepata mchumba halafu maisha yako kiroho yanadidimia ujue huyo si wa kutoka kwa Mungu.

SHERIA YA TATU
NAFSI NI KIGEUGEU NA HAINA MSIMAMO
Mtume Paulo anasema kuna jambo hataki kulifanya lakini hujikuta anafanya RUM 7:16-19 Nafsi inapokumbana na jambo zito hugeuka, YUSUPH alipojua Maria ana mimba nafsi yake iligeuka na kuamua kumwacha Mungu asingeingilia kati Maria angekuwa ameshaachwa Mt 2:19 -20 Ukiongozwa na nafsi kila msichana ukimwona utamwambia nataka kukuoa.

SHERIA YA NNE
NAFSI HUKINAISHWA
Kwa kawaida nafsi ya mtu kabla haijakipata kitu huwa na shauku kubwa sana na ikishakipata huwa inakinaishwa nacho na kutamani kingine kipya au kizuri Zaidi.mf simu.Pia ukioa au kuolewa kwa msukumo wa nafsi ukikinaishwa na mwenzako unadhani nini kitafuata? Roho wa Bwana anapokupa mwenza hutakinaishwa naye kwa maana anakuja na upako wa Mungu na matunda ya Roho mt mf Ibrahimu aliishi na Sara mpaka uzeeni japokuwa Sara alikuwa tasa.Adamu aliishi na Eva kwa miaka 900

SHERIA YA TANO
NAFSI INAWEZA KUPINGANA NA MAPENZI YA MUNGU
Hebu tazama Yesu katika mafundisho yake alisema yampasa kufa kwaajili ya watu lakini muda ulipofika alisema baba ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke nafsi ilikuwa inapingana na mpango wa Mungu MT26:38-39 Lakini alipogundua kuwa anapingana na mpango wa Mungu akasema si kama nitakavyo mimi bali mapenzi yako yatimie.mf wa MARIAM LK1:38 hata Sara pia Mw18:9-15

SHERIA YA SITA
NAFSI HAINA IMANI
Kuna uwekano Mungu ameongea na wewe lakini nafsi inakataa kuamini Mdo 12:5-14 wakristo waliomba Petro aachiwe aliachiwa wanakosa Imani.Pia Yoh11:20-27.Kumbuka usiangalie watu wanasemaje bali angalia Mungu anasemaje?
Mungu asipohusika, utajikuta unasema uko sawa wakati unavuja chozi usiku na mchana.

SHERIA YA SABA
NAFSI HUCHUKIA NA KUFURAHI
Nafsi inaweza kukufanya umchukie uliyeletewa na Mungu na kwa sababu haijaridhika naye kwa vigezo vya kimwili.Kumbuka Mungu anapomleta mtu kabla ya kuisikiliza nafsi yako msikilize kwanza yeye MUNGU hakulazimishi wewe umpende mtu huyo bali akikuletea mtu hata kama ulikuwa humpendi atatoa kibali kwenye nafsi yako umpende.kumbuka sio kila maombi yanapata majibu kutoka kwa Mungu majibu mengine yanatoka kwa nafsi.Nafsi inapenda sana kusifiwa naikitokea kila siku mtu ankuambia wewe ni mzuri maneno haya yakirudiwa mara kwa mara nafsi huyapokea na kuyapenda.Mtu akikusifia usirembue macho bali mpe sifa Mungu

SHERIA YA NANE
NAFSI INAJUA KUPENDA
Rej Mark 12:30-31 nafsi hupenda kwa sababu, na kitu inachokipenda kikitoweka upendo huisha pia KAMA UNA MCHUMBA JIULIZE kitu gani kinakufanya umpende na je kikiondoka upendo bado utakuwepo

(5)Usimkubali bali mchunguze
Wapenzi neno la Mungu linasema msizikubali kila roho bali mzipime 1 Yoh4:1-2 Mtu akikufuata utampima kwa kuangalia sheria za nafsi utajua kama anaongozwa na Roho au nafsi.Pia fanya maombi muulize Roho kama huyo mtu anatoka kwake na kama sivyo kemea ashindwe kwa jina la Yesu na ,Na wakati unaomba kibali cha Roho mt usimshirikishe omba peke yako

(6)Jiulize maswali yafuatayo na uyapatie majibu
Swala la kuoa na kuolewa ni agano na si mkataba uchumba ni mkataba lakini ndoa ni agano :-
1. Je atakuwa msaada wa kiroho kwangu? Kusudi kuu la Mungu kila mtu aingie mbinguni Ez18:23-24,Yoh 3:16, kuna watu wamekufa kiroho baada ya kuoa na kuolewa .angalia Mke si msaidizi wa kuosha vyombo nk ni msaidizi wa kufika mbinguni.Delila hakuwa msaada wa kiroho kwa Samson Waamuzi16:4-22

2. Je Imani yetu inafanana? Tofauti ya kiimani huathiri ndoa na maisha ya watoto kiujumla tofauti ya kiimani huweza kuleta migogro baina ya familia Malezi kwa watoto yatayumba tu. Mf 1falme19:1-3 ,Mith 22:6

3. Je maongezi yake yanamwinua Kristo? Kumbuka ukitaka kujua tabia ya mtu angalia rafiki zake na maongezi yake .Yale anayoongea ndiyo yanaujaza moyo wake. Moyo ulio na kristo utaongea habari za Kristo na moyo wa shetani utaongea uzinzi na umbea

4. Je ni msaidizi kweli? Mw 2:18 usaidizi si wa kazi wakati wa Adamu hakukuwa na sahani na masufuria wala mashamba ya kulima usidizi ni wa kiroho.Msaidizi wako mtafanana kimawazo.

5. Je amezama katika Kristo? Kuzama katika Krsto si kufanya huduma za kanisa pekeyake bali ni kuishi kadiri impasavyo mkristo

6. Je mawazo yenu yanafanana? Ikiwa mawazo hajafanana ni rahisi sana kutokea ugomvi ,mfano mume anapenda aina Fulani ya watoto na mwanamke vilevile

7. Je unapoongea naye unakua kiroho? Je unapokuwa naye unapata hamu ya kusoma neon la Mungu?

(7) Angalia mazingira mliyokutana, je ni kanisani? bar? disco? Au kwenye kwaya au kikundi cha sala? Je kama umempenda sababu anaimba vizuri siku akiacha kuimba itakuwaje? Ujue unaoa mtu na sio kipaji Mf wa dada aliyepooza baada ya ajali.Hakuna kitakachotutenga na upendo wa Kristo Rum8:35-39

MAISHA YA UCHUMBA
MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUKWEPA VISHAWISHI WAKATI WA UCHUMBA
 Zawadi zenye hisia za mapenzi
 Kuagalia picha za mapenzi
 Epuka mazingira ya hatari
 Epuka maongezi yanayochochea mapenzi
 Epuka kushikanashikana
Zawadi zisitumike kama mtego wa kupelekana katika vishawishi. Zimetumika sana kuwavalisha miwani ya kuona karibu wakati tunatakiwa kuona mbali. Waichana baadhi wamejikuta wakitoa zawadi  ya ngono ili kulipa fadhira za wavulana wao.


JINSI YA KUISHI MAISHA MATAKATIFU YA UCHUMBA
 Kaeni eneo la wazi
 Kila mnapokutana fanyeni maombi
 Mkikutana someni neno la Mungu
 Peaneni ujumbe wa neneo la Mungu na sio mapenzi
 Pangeni mipango ya maisha yajayo
 Jadilini suala la kazi
 Jadilini suala la watoto
 Msishirikiane kimwili kabla ya ndoa

MAMBO MUHIMUYA KUJUA KABLA YA KUOA NA KUOLEWA
 Mfumo wa maisha yako utabadilika
 Marafiki watabadilika
 Maumbile yatabadilika
 Majukumu yataongezeka
 Jiandae kuwa kiongozi

USHAURI
 Usioe au kuolewa sababu ya kuiga
 Jiandae kabla ya kuoa na kuolewa
 Usifanye haraka kuoa au kuolewa
 Usioe wala kuolewa kwa( kulazimishwa
 Kaa na Mungu vizuri


MWENYEZI MUNGU AKUSAIDIE UUTAMBUE WITO WAKO NA AUPALILIE ILI UWEZE KUUFIKIA MUNGU AWABARIKI NA NAWAPENDA SANA
REFERENCE
1. HOLY BIBLE
2. Mwl Joseph Urio
@
Dr Godbless Emeritha Nicetus Massawe
Bachelor of Veterinary Medicine 2011-2016
0752684380
AD MAJOREM DEI GLORIUM (For the greater glory of God)

Edited by  Eng Herman Nguki wa Malekela.
www.ngukiherman.blogspot.com
0763639101/0679639101
Thank you very much for visiting my blog. In case you don't see other topics, just click home/ view the web version, it will display the home page and topics list which have been categorized by months posted. You are welcome. Share and comment, questions will be answered. Eng Nguki

14 comments:

  1. Amen be blessed brother Herman Nguki Wa-Malekela

    ReplyDelete
  2. Stay blessed brother, I like it,na Mungu atusaidie

    ReplyDelete
  3. Thax brother be blessed a million...
    KUNA KITU NIMEDAKA HAPO

    ReplyDelete
  4. "Mungu asipohusika, utajikuta unasema uko sawa wakati unavuja chozi usiku na mchana." Kweli utajikuta ujilazimisha kufurahi lkn uhalisia wa furaha haupo.

    ReplyDelete