Halahala mti na jicho |
Potelea mbali, ndio, potelea mbali. Wapi huko? Sijuwi hata mimi.
Naam. habari ya wakati huu ndugu yangu, Siku moja mama mmoja akaniomba niongee na binti yake wa miaka 18 ambaye yuko kidato ch tano kwa maana anaona tabia zake zimeanza kuwa ndivyo sivyo na yeye anajitahidi kuongea naye lakini haoni mabadiliko. Huyooooooooooo hadi nyumbani kwaao. Nikakaa mahali pa utulivu kabisa na kuanza kupiga stori. Nikaanza na utani mwingi na comedy ndani yake huku nikitaka kujua mwanzo wa hizi sarakasi, anapenda nini, hapendi nini n.k.
NILIYOYAPATA
Miaka miwili iliyopita dada yake ambae yupo chuo kikuu alikwa hapa nyumbani na alishakuwa na mahusiano na wanaume wa kuhusiana naye huko chuoni na pia hapa nyumbani. Dada alikuwa anaongea kwenye simu na hawa wanaume kwa nyakati tofauti bila kuwachanganya. Dada alikuwa akimsimulia waziwazi anavyofarijiwa na kupewa anavyohitaji kwa wanaume hawa. Muda mwingi alikuwa akisoma message za watsapp na hizi za kawaida au kuongea na simu, basi alitabasamu na kumpa mshawasha mdogo wake kujua kulikoni, ambapo dada jibu lake lilikuwa 'mdogo wangu kuwa utayakuta, it is more than sweet'. Wakati mwingine alikuwa anamuuliza dada yake 'sasa muda wa kuolewa atafanyeje na haoni kama anamkosea huyo mme atakayekuja kumuoa'. Dada alikuwa akiangua kicheko na kumuambia ataelewa mara muda wa kuonja ukifika,kwa maana wanaume wote wanafanya ngono sana tu, tena wao huwa hawagunduliki hivyo hutumia hiyo nafasi kufanya uchafu mwingi, hivyo kwa msichana anayejidanganya eti hafanyi ngono kwa kuwa ataolewa na mvulana ambaye hajawahi kufanya ngono anajidanganya, vinginevyo ajiumbie huyo mwanaume mwenyewe ni bora tu afanye, but awe makini sana kusiwe na madhara, kama mimba na ukimwi. Na ikitokea bahati mbaya kapata kati ya hivyo au vyote, POTELEA MBALI KWA MAANA MATATIZO YAPO KWA AJILI YA WATU NA YEYE HATA KUWA MTU WA KWANZA KUYAPATA HAYO, BADO MAISHA YANAENDELEA KWA MAMIA YA WATU AMBAO WALIFURAHIA MAPENZI. Tena kuna watu walijifanya kuwabania wavulana wanaowapenda eti hawataki kufanya mapenzi, lakini mwisho wa siku wakaja kuolewa na mijanadume milevi na mihuni isiyojari na pengine ukaenjoy kwa muda mfupi tu na kufa kwa presha au magonjwa. Bora nini sasa? Ni bora tu kufurahia maisha yamapenzi, na pia akamwambia ukishaanza sio rahisi kuacha.
Hivyo na yeye mwaka jana wavulana walianza kumtongoza wengi kama nyuki, kwanza aliona ni usumbufu ulioibuka ghafla, na bora amkubali mmoja ili kupunguza usumbufu kwa wengine, ikawa hivyo, akaendelea na kwa kuwa aliambiwa akianza hawezi kuacha, hivyo hata alipoenda rikizo kwa bibi yake akitongozwa alijitahidi angalau kumkubalia mmoja ili mambo yaende, na hadi sasa wanagombana na mama yake kwakuwa anambana sana na kutompa muda wa kuwa huru ili akaonane na mmoja kati ya wapenzi wake. Na naamini kuwa akiacha moyo utaumia sana na pengine mambo mengi hayataenda sawa.
Tuliongea mengi sana, ambayo yalinipa picha kamili ya kilemba cha ukoka alichovalishwa yule binti na dada yake na kujikuta anageuka mtumwa wa ngono na kujidanganya kwa kusema anawapenzi kumbe anawafanya ngono wenzake. Nilimshauri mengi sana na kumuhakikishia kuwa yeye ni binadamu aliyekamili, kuwa na hisia sio dhambi, bali ishara ya ukamilifu, na kamwe sio tiketi ya kufanya ngono, shule na ngono haviendi, sala na ngono haviendi, lazima useme HAPANA yenye kumaanisha hutaki kuwa chombo cha starehe, jiheshimu jisitiri, jitawale, furahia ujana wako kwa kufanya mambo mema.
Ni kweli mtu akifanya ngono hata kuwa mtu wa kwanza, kama kulivyo kufa, mtu akifa sio yeye wa kwanza, swali linakuja Mungu alikuumba ili uje upotee kirahisi hivi jamani? Na wewe msichana aliyekwambia kuwa wavulana wote wanafanya ngono ni nani? hizo takwimu mwenzetu ulizikusanyia wapi? Bila shaka umeanza na wale ambao wamefanya na wewe, au kwakuwa wengi wamekutongoza basi unajua kilakijiji, kila kata, tarafa. wilaya na mkoa na nchi nzima wanafanya ngono? Unajidanganya. Wenye akili wamejitoa sadaka kuishinda tamaa ili waje kufurahia katika ndoa? Ishu ya nitaolewa na nani, muachie Mungu aliyekuumba ndiyo anajua ubavu wako uliko na ndiye aliyeutoa, sasa wewe kilanga chako cha kuvania maubavu ya watu, ukija na ule wa kwako utauweka wapi? Au mbavu nyingine unataka kutengeneza mishikaki ule? Muache Mungu afanye yake kwako, usifanye ngono hadi siku ya ndoa, huwezi kuugua huwezi kuwa chizi, bali utakuwa na nafsi ya kutafakari vizuri namna utakavyofurahia tendo la ndoa ndani ya ndoa.
Ishu ya kutongozwa na wengi pia ni kawaida tu kwa maana kila mtu anavutia, na wakati mwingine watu wanakujaribu tu, na wewe kichwakichwa unaingia kukaa kwa mashabiki wa Yanga wakati umevaa jezi ya Simba, mimi simo yatakayokukuta huko.Wavulana wenyewe wanatongozwa sasa wewe unshangaa nini? KATAA KWA KINYWA CHAKO DADA. Kwa taarifa yako, maisha ya kujitawala bila kufanya ngono ni sala, kwamba unamuomba Mungu akuletee anayejilea kama wewe. Na ukisema huwezi kuacha basi ni shwangwe na vigeregere kwa shetani kwa maana atakuja mfanyangono sugu ili chuma kinoe chuma., Kama huamini endelea, na UTANIKUMBUKA NGUKI MIMI.
Wakati fulani hata wavulana nimekuwa nikiwasikia bila aibu wanasema wasichana wote wanafanya ngono na kwamba kama haufanyi ngono kwa kudai eti utakuja kuoa msichana ambaye hajawahi kufanya ngono basi ni ndoto za mchana. Labda ujiumbie wewe mwenyewe. Mnaumwa nyinyi wenye hayo mawazo, MBONA MNALIPA KISASI KWA MTU MSIYEMJUA? ni dhambi hiyo. Wewe ni nani ambaye umeshajua utaoa mtu wa aina gani? au ndio sala yako? unadhani kwasababu kila msichana unayemtongoza anakubali tena unamkuta wewe sio wa kwanza basi wote ni hivyo? NI MUNGU TU ANAWAEPUSHA WALIO SAFI ILI USIWACHAFUE WAKUTWE SAFI NA WASAFI WENZAO WAFURAHIE NDOA TAKATIFU. Pole unayezidi kujichafua, hata hivyo una nafasi ya kuanza mfumo mpya wa maisha na ndio maana kuna wengine tendo moja la ngono linawapa matatizo yote na pengine kifo, wewe umebaki mzima kwa maana Mungu alijua kua siku utabadilika tu, huenda ikawa ni leo hii.
Subiri muda ufike, mfunge ndoa na kuvishana pete za ndoa ishara ya ulinzi kutoka kwa mwenzi wako ambapo matokeo ya tendo la ndoa kila mtu atayapokea kwa furaha. |
HATA MIMI NINA HISIA KALI
Ikumbukwe kuwa hatuachi ngono kwaajili tu ya mke au mme mtarajiwa, bali ni kwaajili ya afya yako na ustawi wa maisha yako pia mfumo wa kufikili na kutenda kazi za kawaida za kijamii unakuwa na ufanisi mkubwa sana kwa mtu asiyefanya ngono. Hata mimi Nguki usidhani naandika haya labda mwili wangu umelala, ah, weeee, hisia zipo tu tena kali sana kwa maana nipo kamili kijinsia na kila kitu. Je hiyo ni tiketi kwamba nitafute mtu wa kufanyanaye ngono?, hapana. Huwa nafanya nini sasa mwili ukiwaka????? Sikia
- Kwanza nafurahi na kumshukuru Mungu kwa maana ni ishara kuwa nitakuwa mtendaji mzuri wa wizara ya mambo ya ndani from the wedding night.honeymoon etc.
- Ninajiambia kuwa mimi sijaoa bado, na pia kuna mtu anajinyima kwaajili yangu na Mungu kaniandalia.
- Ninajiambia kuwa hisia hizi atakuja mtu sahihi ,tutahudumiana muda wote sahihi na mazingira sahihi.
- Ninajiambia kuwa matokeo ya ngono sasa ni fedheha, aibu, na kuwahuzunisha wazazi, walezi na jamii kwa ujumla.
- Ninajiambia nataka kuwa baba bora wa familia yangu muda ukifika, ishu ya kwamba mke wangu atakuwaje hayanihusu, Mungu aliyenimba anajua, kazi yangu ni kusali na kufanya uchaguzi sahihi wa kuomba mahusiano,.
- Ninajiambia pia kuendekeza hisia hizi zikiniendesha na kufanya ngono sasa naweza kujikuta napata magonjwa ya ajabu ajabu na madhara mengine ambayo yanawezaa kuniua, hata kama nitasema potelea mbali mimi sio wa kwanza.
- Kwa kifupi sigombani na mwili wangu kwa maana mimi ndiyo mwenye hatimiliki ya mwili wangu na mtoa maamuzi, hivyo nauambia huna chako kwa sasa, hadi siku ya ndoa.
- Nabaadilisha mazingira niliyokuwepo kwa wakati huo, najiweka busy kusoma vitabu na mambo mengine mengi ya kijamii na kidini hivyo kuhamisha kabisa mawazo, na pengine namuuliza mama kama kuna vitu vya kufuata sokoni ili niende kuvinunua na kubadilisha mazingira..
Tena hata sio lazima yote yafanyike kwa pamoja, mwili unapoa wenyewe nakuhakikishia. Kwa mtu aliyezoea ngono anashangaa kuwa labda nasema nadharia, badilika, vinginevyo unajichimbia shimo la kukufukia mwenyewe na kizazi chako, kwani mdogo wako hasa wa kike akiwa anafanya ngono na limwanaume fulani barabarani huko unachekelea na kumpongeza? na binti yako je? Badilika sasa, kwa wa mfano. Hata wanaokuona wewe ni mhuni wanaweza kuanza kukuheshimu na kukupa nafasi ya kukuamini, na Mungu atawaaminisha kuwa wewe sio yule wa zamani. Anza leo kuamini kuwa wewe ni wa muhimu sana na you will have a wonderful moment with your wife/husband in the marriage. Usiseme Potelea mbali, utapotea wewe mwenyewe na kizazi chako,wala sio mtu mwingine.
NAKUTAKIA TAFAKARI NJEMA. Kama una swali usisite kuniuliza hapo chini, au kama unataka ushauri binafsi, nitafute kwa simu au email, watsaap nipo kwa hiyo number ya voda.
Eng Nguki Herman. MEmail: ngukiherman@ymail.comInstagram: @eng.ngukiwamalekelaTwitter: @engngukiherman
UCE Tanzania Volunteer.
nice lesson bro
ReplyDeleteAmen. Tuko pamoja
DeleteAsante sana kwa somo zuri la usafi wa moyo
ReplyDeleteMungu akubariki pia kwa kusoma na kuelewa
DeleteAmina
DeleteKaka hii nikarama, kwakweli sijawahi soma makala nisichote kitu, kazi nzuri mungu aZidi kukupanguvu na kukufunulia zaidi
ReplyDeleteAmina kaka Elius. Utukufu kwa Mungu
Deleteubarikiwee kwa kutupa ujumbe mzur
ReplyDeleteAmina, tuko pamoja dada
DeleteNimeelewa be blessed
ReplyDeleteAsante my dada Lucy. You are welcome
Delete