Wahitaji wanakutegemea wewe, jifunze kuhudumia makundi maalumu |
Nakumbuka wakati niko mdogo, tena nikiishi katika familia ya kipato cha chini sana, bibi alijitahidi sana wakati wa sikukuu hasa Krismas na Pasaka angalau kupika wali ili majirani wenye uwezo watakavyoanza kunukisha vyakwao basi nisijisikie vibaya, au kuingia kwenye mtego wa kuchoropokea huko, si unajua tena utoto. Lakini ni ukweli usiopingika kwamba pale unapokuwa na uduni fulani au kuishi maisha magumu unaishi kwa hofu na kuona watu wote hawakupendi (defensiveness). Ikitokea mtu fulani kajitolea kukusaidia nawewe ufurahi angalau siku maalumu kama sikukuu, hakika unatenga muda wa ziada kusali kwaajili yake ili afanikiwe zaidi.
Logo ya Jumuiya ya Sant' Egidio |
CHRISTMAS LUNCH NI NINI?
Chama cha kitume cha Sant' Egidio kilicho chini ya Kanisa Katoliki kinawaita waliobarikiwa kuwa na uwezo kidogo kuliko wenzao ili kujitoa kuwasaidia wahitaji. Ninapozungumzia uwezo sijasema pesa pekee, bali hata kusali kwaajili ya wengine, kujitolea muda kwaajili ya kuwasaidia wengine kwa huduma, faraja na sala. Miongoni mwa misingi au nguzo ya jumuiya hii ni sala na huduma. Kwenye kipengele cha huduma hii inahusisha kwenda kuwatazama wagonjwa majumbani au hospitalini, kuwatazama wafungwa na wakimbizi. Unaenda kusali nao na kama una zawadi yoyote bila kujali ni ndogo kiasi gani, kwa maana Mungu aliyekuwezesha kuvipata anajua vyema kuliko wanadamu wanaokutazama kwa nje.
Kwaajili hiyo chama hiki cha kitume huandaa chakula cha mchana kila tarehe 25 Desemba na kuwalisha makundi ya wahitaji mahali pale walipo, kuwapa zawadi na kufurahi pamoja nao. Makundi haya huhusisha watoto ytima, wazee, walemavu na watindiwa ubongo. Mfano kwa chuo kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) wao huwakusanya wahitaji kutoka nyumba ya wazee na wasiojiweza Fungafunga, vituo vya watoto wenye ulemavu wa mwili na akili Mehayo na Amani, Kituo cha watoto cha Rosalia wa Sowano nakadhalika.
Ninaposema wahitaji wote ieleweke ni WOTE bila kujali dini wanazotoka wala kituo kiianzishwa na watu gani.
Upendo wa Mungu hudhihirika katika nyuso za wahitaji pale wanapokumbatiwa na kuambiwa wanapendwa na wana nafasi ya kuendelea kuishi. Ikumbukwe huduma ya namna hii sio ya kikundi fulani pekee, hapana watu wa dini zote wapo walemavu na wahitaji. vivyo hivyo suala la kujitoa kwa wahitaji halina mipaka.
Kama unapata shida sana kuelewa suala la Christmas Lunch , tumia simu yako au Computer yako nenda kwenye google na undike CHRISTMAS LUNCH OF SANT' EGIDIO , utaletewa video na maelezo ya jinsi tukio hili linavyofanyika nzhi mbalimbali duniani kwa maana sio Tanzania pekee, na utagundua unachelewa tu kuungana na kundi kubwa la watu linalojichotea neema kwa Mungu kila uchwao kwa kuwasaidia wahitaji.
Viongozi wa jumuiya za wanafunzi wakatoliki vyoni TMCS na jumuiya ya Sant' Egidio wanahangaika kila kona kutafuta michango kila kona ili kuwezesha utoaji wa chakula hiki cha mchana anagalau kila mhitaji apate sahani moja ya chakula siku ya Christmas. Wapo wachache, na hawawezi kufika kila mahali kuhamasisha, ikumbukwe ni wanafunzi na wanabanwa na ratiba za chuo, lakini uwe mwanafunzi au sio mwanafunzi unaweza kuchangia leo hata kuwalisha wahitaji wawili tu siku hiyo kwa njia rahisi nitakayokwambia leo humu.
Jumuiya inajitahidi kupandikiza moyo huu wa huruma kuanzia kwa vijana wadogo kabisa ili wakue huku wakitambua kuwa wajibu wa kusaidia wahitaji ni wa lazima kwa kila ambaye Mungu kamuweka hai. Hii itapunguza unyanyasaji na pengo kati ya walio nacho na wasio nacho. Hebu fikiria wewe binafsi ikitokea kuna sherehe fulani muhimu, ukajiandaa vizuri sana na kusafisha viatu vyako kisha kuviweka nje vikauke vizuri. Dakika chache kabla ya shamrashamra kuanza unagundua viatu vyaki nje vimeibwa na hauna viatu vingine, hivyo utalazimika kuvaa malapa au ubaki ndani umejifungia kwa maana wenzako wote wameulamba vizuri nje huko. Yote tisa, la kumi anatokea mtu anaviatu jozi mbili au tatu, na unamuangalia kwa jicho la huruma lakini hakuelewi, unamwambia shida yako, lakini anakuambia hivi vingine atavivaa wiki ijayo hivyo hawezi kumgawia mtu. Sijuwi utawaza nini au utajisikiaje
JE UNGEPENDA KUUNGANA NA MAMIA YA WATU KUCHANGIA CHRISTMAS LUNCH YA MWAKA 2016?
Nirahisi sana. Mchango wako wa kiasi chochote utakaotoa utafanya mambo yafuatayo:
Kama unapata shida sana kuelewa suala la Christmas Lunch , tumia simu yako au Computer yako nenda kwenye google na undike CHRISTMAS LUNCH OF SANT' EGIDIO , utaletewa video na maelezo ya jinsi tukio hili linavyofanyika nzhi mbalimbali duniani kwa maana sio Tanzania pekee, na utagundua unachelewa tu kuungana na kundi kubwa la watu linalojichotea neema kwa Mungu kila uchwao kwa kuwasaidia wahitaji.
Wengine hawana miguu wala mikono, hivyo wewe ndio wakuwachukulia chakula na kuwalisha kama ambavyo hapa dada Dorice Stanford anavyofanya katika Christmas Lunch ya jumuiya ya Sua |
Sio Tanzania tu hata Burundi, Malawi na nchi nyinginezo wanajitolea kufanya huduma hii, hata wewe waweza ifanya kama sehemu ya kumshukuru Mungu. Anza leo. |
Uwe sauti yao. Uwezo unao. kidogo ulichonacho gawana na wahitaji. |
Nirahisi sana. Mchango wako wa kiasi chochote utakaotoa utafanya mambo yafuatayo:
- Usafiri kwenda na kurudi kuwachukua wahitaji kutoka katika vituo vyao na kuwaleta eneo moja. Hawa ni wazee, watoto na walemavu kutoka Fungafunga, Mehayo, Amani Center na Kihonda.
- Mapambo ya ukumbi.
- Chakula na vinywaji kwa wahitaji tajwa hapo juu.
- Zawadi kwa wahitaji ambapo baada ya chakula kila kituo hupewa zawadi kama unga, mchele, mafuta, maharage na vifaa vya shule kwa watoto wanaosoma.
Mungu wa mbinguni anatambua uwezo wako kuwa ni mdogo, na anakuhitaji ujitoe kwa pale utakapoweza. Jitoe tafadhari. Nakutakia tafakari njema kwa hayo machache niliyokushirikisha, naamini utaungana nami kuhakikisha hili linawezekana. Waweza kumhudumia hata mzee au mlemavu mmoja tu au familia fulani isiyojiweza hapo karibu na kwenu. Sasa usikubali shetani akupige mtama ukaanza kusingizia eti hakuna wahitaji karibu na kwenu, hapo utakuwa unamtukuza ibilisi ambaye ni baba wa uongo.
Asante kaka, nivema kujumuika sote kuwachanzo cha furaha kwa wengine na ndio dini ya kweli kuwasaidia masikini.
ReplyDeleteAsante sana mkiti, tuko pamoja
DeleteAsante mtumishi wa mungu kwa kutukumbusha majukumu yƩtu na ndio kusudi la mungu kutuumba tofauti tofauti ili tuweze kusaidiana!
ReplyDeleteAmina. Tuzidi kusonga Mbele
Delete