Tumsifu Yesu Kristu, leo hii natamani nikushirikishe kitu juu ya nguvu ya Novena. Bila shaka kwa Mkristo Mkatoliki neno hili novena sio geni, wala sihitaji kulidadavua kirefu. Kwa kifupi NOVENA NI SALA YENYE NGUVU ISIYOSHINDWA KAMWE KUTOA MAJIBU IWAPO UTASALI KWA IMANI. Zipo novena nyingi kama za Roho Mtakatifu, Pentekoste, za watakatifu kama Rita wa Kashia nakadharika. Kwa wanafunzi wa chuo novena ya Roho Mtakatifu najua lazima huwa inakumbukwa kipindi cha kukaribia mitihani. Ipo pia novena ya kushukuru baada ya kufungua chuo kwa kumshukuru Mungu kwa kurudi salama na matokeo ya kukuwezesha kuvuka mwaka, japo hii wengi huwa wanaipuuzia kwa kuwa hakuna wanachokiomba, walishapata tayari vyote.
Lakini kwa waliopo au waliotoka jumuiya ya TMCS SUA-New Hostels, tangu mwaka 2014 tulianza kusali Novena kwa Mt Rita wa Kashia ambayo huchukua siku 12, yaani kuanzia Jumatatu ya kwanza ya UE hadi Ijumaa ya mwisho ya UE kwenye vipindi vya sala za asubuhi. Yaani siku 9 za novena na 3 za shukurani, zote zipo ndani ya muongozo wa vitabu vya Mt Rita wa Kashia. Mara zote huanza na sakrament ya Kitubio. Novena ile kwa wenzangu ambao tumekuwa tukishiriki wote ni mashahidi, kila mtu kwa nafsi yake, Mungu amekuwa akijibu kwa upekee sana yale maombi takribani 15 kwenye muongozo wetu. Hakika Mungu atukuzwe.
AMENIJIBU TENA KWA MAOMBEZI YA MT RITA WA KASHIA
Kama binadamu mwenye malengo na mahitaji, niliazimia tena kujichotea baraka zilizopo bure kwa Mungu wetu kupitia maombezi ya mtakatifu huyu shujaa wa kujitoa sadaka ambapo tarehe 9/9/2016 nilianza novena kwa Mt Rita wa Kashia nikiwa na mahitaji 10 ambayo niliyaorodhesha kwenye karatasi yangu. Katika orodha yangu kulikuwa na shukurani na maombi. Yale maombi yalikuwepo yale ambayo majibu yake ni tangible (yani yakijibiwa nitajua moja kwa moja) na yalikuwepo ambayo ni intangible (siwezi kuthibitisha kwa macho kuwa kayajibu lakini kwa imani). Novena ile ilianza tar 9/9 Ijumaa na kwenda hadi 20/9/2016 na kukamilisha siku 12. Nilianza nikiwa Iringa nyumbani lakini tar 18/9/2016 Jumapili nilisafiri kwenda Mbeya kwaajili ya semina kwa wiki moja, hivyo niliimalizia nikiwa Mbeya.
Mungu anashughulika na mambo yetu usiku na mchana, wema wake watuzunguka pande zote |
MAAJABU.
- Baada ya kuanza novena tarehe 9/9/2016, kesho yake tarehe 10/9/2016 ombi la kwanza kuorodheshwa likatimilika vilevile nilivyoomba.
- Siku ya 7 ya novena yaani 15/9/2016 ,Ombi la pili kuorodheshwa kwenye karatasi yangu likatimia vilevile nilivyoomba na kuandika.
- Siku ya 10 ya novena tar 18/09/2016 Ombi la tatu kwenye orodha yangu lilitimia kwa mfumo uleule. Nilistaajabu mno, maana ombi hili niliwaambia hata baadhi ya marafiki zangu kuwa nimelifungia novena na lazima niibuke kidedea, likatimia vilevile.
- Baada ya novena kuisha, Mungu aliendelea kujibu orodha yangu ambapo yale tangible lilibaki moja ambalo ni la muda mrefu (long term goal) ambalo naamini Mungu ameshajibu lakini anasubiri tu siku nzuri ya kuniambia ili nipokee. Na yale ambayo siwezi kuona majibu kwa macho naamini Mungu ameshajibu yote kwa maombezi ya mama huyu Rita wa Kashia ambaye Kanisa katoliki kwa kusaidiana na shirika la Mtaktifu Agustino tunamuita MTAKATIFU WA MAMBO YALIYOSHINDIKANA NA MFANYA MIUJIZA MTEULE WA MUNGU.
- Watu wengi pia wameendelea kushuhudia mambo makubwa na yaajabu ambayo Mungu amejibu kupitia maombezi ya Mt Rita wa Kashia.
Hakika nakosa cha kusimulia zaidi, lakini jinsi Mungu alivyojibu tena kwa mtiririko uleule kama nilioandika kwenye karatasi yangu ya maombi, kweli niliamini Mungu yupo na anajibu waziwazi na tunajionea kwa macho.
LINI TUNASALI NOVENA KWA MT RITA WA KASHIA?
LINI TUNASALI NOVENA KWA MT RITA WA KASHIA?
- Kuanzia kila Jumatatu ya kwanza ya mwezi. Siku ya 12 (ya mwisho) inadondokea Ijumaa ya wiki la pili la sala.
- MAALUMU KWA MWEZI WA MAY. Mt Rita wa Kashia alizaliwa Jumamosi ya 22/5/1377 na kufariki Jumamosi ya 22/5/1457. Hivyo kwa upekee wa mwezi huu wa tano NOVENA HUANZA SIKU 9 KABLA YA 22/5 AMBAYO NDIO SIKU YA KUMBUKUMBU YAKE (feast day), yaani tunaanza novena tarehe 14/5 ili siku ya 9 idondokee siku hiyo ya 22/5. Ukiongeza na siku tatu za shukurani (kwa mujibu wa muongozo) novena itakamilika tarehe 25/5. Tarehe hii 22/5 ni siku kubwa sana kukumbuka matendo makuu ya Mungu kupitia mteule wake huyu mkuu, ambapo kuanzia Kashia na dunia nzima misa mbalimbali hufanyika kwa heshima ya Mt Riata wa Kashia
- Waweza kusali wakati wowote unapokuwa na nia yoyote iwe shukurani, maombi ya kawaida, mfadhaiko mkubwa au changamoto nakadhalika. Usisahau pia kusali sala mbalimbali kupitia yeye. Jambo la msingi hakikisha unapata kitabu cha sala na novena.
Nisikilize ndugu yangu hapa chini |
USHAURI WA BURE
Mungu wetu ni tajiri, na vyote tunavyovitamani kwa haki ni vyakwake na sisi ni warithi wake (Rum 8:17, Gal 3:29, Tito 3:7) kwa maana hiyo tukiomba kwa imani anatustahilisha kuvimiliki si kwa sifa za duniani. bali kupokea kwa saburi, unyenyekevu na kuhudumia wengine. Wakati fulani Mungu anaweza asijibu maombi kwa wkati, lakini pengine anakuwa ameshafanya typing , anayo softcopy, hivyo yuko mbioni kuprint ili ukabidhiwe kwa maana anafahamu softcopy huna facility ya kuhifadhi. Sasa ukianza kulalamika na kuona kama Mungu hayupo utamtibua na kumfanya aahirishe kumtuma Malaika Gabiel kwenda stationary kuprint ujue. Tulia, kuwa mnyenyekevu, kuwa na subira, mchukie shetani na matendo yake, jitahidi kupenda kuhudumia kuliko kuhudumiwa. Pale unapopata ugumu, washirikishe watu unaowaamini wakusaidie, sio kila mtu wa kumshirikisha kila kitu. Kwa Kristo sisi ni washindi, kwa Kristo tuko salama. TUMSIFU YESU KRISTO:
Eng Nguki Herman. M
Soma hapa chini kumuhusu Mt Rita wa Kashia |
Navipata wapi vitabu vya Mt Rita wa Kashia?
Vitabu vya Mt Rita wa Kashia hutolewa na shirika la Mt Augustino ambalo Mt Rita mwenyewe alijiunga na kufanya utume. Viko vingi sana.
Vinapatikana:
Ukitaja tu VITABU VYA NOVENA KWA MTAKATIFU RITA WA KASHIA utapata. Picha zake ni hizi hapa.
Vitabu vya Mt Rita wa Kashia hutolewa na shirika la Mt Augustino ambalo Mt Rita mwenyewe alijiunga na kufanya utume. Viko vingi sana.
- Vipo vidogovidogo vitatu (Cha novena pekee, cha sala kupitia kwake na cha maisha yake).
- Kipo kimoja kinachounganisha vyote vitatu hapo juu (Mt Rita wa Kashia-Waridi lenye Kunukia) (three in one-NI KIZURI ZAIDI)
- Kipo cha maelezo na sala mchanganyiko
- Kipo kikubwa kuliko vyote (Taji la mawaridi ya Mt Rita) ambacho kina novena na sala kwa mfumo wa kuhiji ( kama upo hija Kashia)
Vinapatikana:
- Popote ilipo nyumba ya malezi ya shirika la wa-Augustino
- Maduka ya vitabu ya majimbo au parokia
- Maduka ya mashirika ya kitawa kama Fransalian, Consolata, OFM Capchin, OFM Conventuary, Daughters of St Paul nakadharika..
Ukitaja tu VITABU VYA NOVENA KWA MTAKATIFU RITA WA KASHIA utapata. Picha zake ni hizi hapa.
Hiki kina novena pekee |
Hiki kina sala pekee kwa Mt Rita |
Hiki kinaunganisha vitabu vitatu (sala, maisha na novena.) Nyuma yake utakuta picha za vitabu vitatu vilivyounganishwa. Ni kizuri zaidi |
St. Rita of Cascia: Patron Saint of the Impossible
May 22 is the feast day of St. Rita. St. Rita of Cascia was an Augustinian nun from 14th century Cascia, Italy. She is the patroness of impossible causes and hopeless circumstances because of her difficult and disappointing life. Through her trials God used her in remarkable ways, not only while she lived, but now from heaven she assists those who plead for her intercession for their own seemingly impossible and hopeless circumstances.
From an early age St. Rita desired to become a nun, but her parents insisted that she marry at the age of twelve. St. Rita did so in obedience to them. Adding to her disappointment, the man her parents arranged for her to marry was cruel and harsh, and she spent 18 years in a very difficult marriage. Her husband eventually became physically abusive, yet she met his cruelty with kindness and patience. Two sons were born to her whom she loved deeply. After many years she eventually won her husband over to greater civility and kindness.
In the 14th century Italy was rampant with warring families caught in a vicious circle of assassinations and bloody vendettas (think Romeo and Juliet). St. Rita’s family was caught up in this strife that was so entrenched in society at that time. Her husband was murdered as a result of the infamous rivalry between the Guelphs and the Ghibellines. St. Rita mourned her husband’s death and interceded for his soul with great earnest.
Celebrating the feast of St. Rita in Cascia, Italy |
Her two young sons, in keeping with the vice of the day, talked of avenging their father’s death. St. Rita did all she could to guide her children into forgiveness, but was unable to dissuade them from their evil intentions. Prayer was her only hope. She prayed that God would change the evil swelling up in the hearts of her sons, or allow them to die before they had the chance to commit a mortal sin and in so doing be separated from God forever. God granted her prayers. Both of her two sons died within a year in a state of grace; they were prevented from following the evil path of their father.
After the death of her husband and her sons, St. Rita was all alone in the world and sought again to enter the convent. She was turned away because of her family’s association with the civil strife; some of the sisters living in the convent were family relations of the men who were responsible for killing her husband. To maintain peace, she was denied entry.
St. Rita, again facing crushing disappointment and yet another impossible situation, had recourse to prayer and the intercession of the saints. St. Rita’s sincerity and spirit of charity and forgiveness prevailed and she was eventually granted entry. She became known as a holy and prayerful nun, often meditating on the sufferings of the crucified Christ.
One day, while praying before a crucifix, St. Rita received a visible wound on her forehead. This was a mystical yet visible mark (stigmata) of Jesus’ wound from the crown of thorns, symbolizing St. Rita’s unity with Christ in his sufferings. She also enjoyed many mystical experiences with Christ during the forty years she lived in the convent. She died on May 22 when she was in her seventies.
St. Rita certainly had a difficult life, but her heartbreaking circumstances drove her to prayer and helped her to become a holy woman. She began her work of intercession for sinners while she lived, starting with those closest to her heart. Through her love and prayers she won the grace of conversion for her husband and both her sons.
Even though her life was full of sorrows and disappointments, she was consoled by being closely united with Christ. He did not abandon her; rather He granted her profound and intimate graces. Now a saint in heaven, St. Rita is the patron of impossible causes, sterility, abuse victims, loneliness, marriage difficulties, parenthood, widows, the sick, and bodily ills and wounds. She is also one of the Church’s incorruptible saints, her body venerated at the basilica named for her in Cascia, Italy.
The incorrupt body of St. Rita at Basilica of St Rita in Cascia, Italy. |
If you are facing a difficult and impossible life circumstance, you can resort to prayer after the example of St. Rita. Below is a prayer to St. Rita as well as a novena. You can also find medals, books, and prayer cards associated with St. Rita here, which make great gifts for those similarly facing difficult and heartbreaking life circumstances.
PRAYER TO ST. RITA
O Holy Patroness of those in need, St. Rita, whose pleadings before thy Divine Lord are almost irresistible, who for thy lavishness in granting favors hast been called the Advocate of the Hopeless and even of the Impossible; St. Rita, so humble, so pure, so mortified, so patient and of such compassionate love for thy Crucified Jesus that thou couldst obtain from Him whatsoever thou askest, on account of which all confidently have recourse to thee expecting, if not always relief, at least comfort; be propitious to our petition, showing thy power with God on behalf of thy suppliant; be lavish to us, as thou hast been in so many wonderful cases, for the greater glory of God, for the spreading of thine own devotion, and for the consolation of those who trust in thee.
We promise, if our petition is granted, to glorify thee by making know thy favor, to bless and sing thy praises forever. Relying then upon thy merits and power before the Sacred Heart of Jesus, we pray thee grant that [here mention your request].
By the singular merits of thy childhood,
Obtain for us our request.
By thy perfect union with the Divine Will,
Obtain for us our request.
By thy heroic sufferings during thy married life,
Etc. {repeat Obtain for us our request after each line]
By the consolation thou didst experience at the conversion of thy husband,
By the sacrifice of thy children rather than see them grievously offend God,
By the miraculous entrance into the convent,
By thy severe penances and thrice daily bloody scourgings,
By the suffering caused by the wound thou didst receive from the thorn of thy Crucified Savior,
By the Divine love which consumed thy heart,
By that remarkable devotion to the Blessed Sacrament,
on which alone thou didst exist for four years,
By the happiness with which thou didst part from thy trials to join thy Divine Spouse,
By the perfect example thou gavest to people of every state of life.
Pray for us, O holy St. Rita, that we may be made worthy of the promises of Christ.
LET US PRAY.
O God, Who in Thine infinite tenderness hast vouchsafed to regard the prayer of Thy servant, Blessed Rita, and dost grant to her supplication that which is impossible to human foresight, skill and efforts, in reward of her compassionate love and firm reliance on Thy promise, have pity on our adversity and succor us in our calamities, that the unbeliever may know Thou art the recompense of the humble, the defense of the helpless, and the strength of those who trust in Thee, through Jesus Christ, Our Lord. Amen.
Saint Rita, advocate of the impossible, pray for us.
Saint Rita, advocate of the helpless, pray for us.
Recite the Our Father, Hail Mary, and Glory Be three times each.
Mt Rita wa Kashia, shujaa wa kujitoa sadaka. Kwa maelezo zaidi sala na tafakari, tafuta kitbu chochote chenye jina la Mtakatifu huyu, vipo vingi sana na vinatolewa na shirika la Mtakatifu Augustino. |
Tanx for sharing,if u won't mind could u tell at least one tangible miracle
ReplyDeleteHahaaaa, no my sister, we can talk more inbox
DeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteAsante kwa ushuhuda mzuri wa kuimarisha imani!
ReplyDeleteAmina,utukufu kwa Mungu
DeleteAsante Nguki
ReplyDeleteAmina kaka Zeno
ReplyDeleteAmina Kaka Nguki.
ReplyDeletePersonally naungana na wewe katika kukubali Nguvu alizijaliwa Mt Ritha wa Kashia katika maombezi.
I really do appreciate her sainthood.
Amina Gerard
DeleteBarikiwa sana mtumishi..hakika huyu ni Mama mwenye Nguvu kwa yalishindikana...
ReplyDeleteAmina Brother
DeleteBarikiwa sana Mtumishi kwa kushare. Kwakweli nimebarikiwa sana.
ReplyDeleteUtukufu kwa Mungu, Tumshukuru Mungu Dada Getrude
DeleteShukrani sana, kwa kuwa nilipata kujua kwa whatsapp kidogo kuhusu Mt.Rita watu walikuwa wakishuhudia nikabidi ninunue kitabu....na hapa tena nimeongezaa ufahamu na umakini...Mungu atusaidie tuzidi kumtafuta na kuiishi imani zaidi siku zote.
ReplyDeleteAmina Dada, ubarikiwe sana na Tumshukuru Mungu
DeletePia kwa maoni yangu ili tumueneze Mt Rita kwa uraisi Duniani kote,naomba wausika waweke sala ya novena yake kwenye INTERNET tuipate kwa uraisi.Nasema ivyo kwani kitabu kinaweza kupotea ata kuliwa na panya kutokana na Maisha tunayoishi.Naomba ndugu tuyatafakari aya mawazo yangu,Amina
ReplyDeleteAmina kaka Mchunguzi, maoni yako ni mazuri sana. Nadhani shirika la Mt.Augustino (Ambao ndio waandishi na wafasili) itapendeza nakifanya hivyo ili kurahisisha upatikanaji hasa ambako hakuna bookshops za Kanisa. Ubarikiwe sana
DeleteKamani iki kilichoandikwa apo juu ndio novena ya Mr.Rita ktk lugha ya Kingeleza?
ReplyDeleteO holy protectress of those who ART in greatest need,
Au amekosea maandishi ya kingeleza kuandika,tizama ilo neno ART ktk hii novena limetumika zaidi ya maramoja nasioni kama linaleta maana ktk Novena,Je nikweri kwamba mwandishi amekosea pia zaidi ya maramoja.
Nashukuru kwa comment kaka. Hiyo ART haijakosewa. Kingereza kina mifumo mingi ya uandishi. Rejea Luka sura ya 11 kwenye sala ya Baba yetu, soma kwenye Bible ya kingereza hasa ile aya ya 2, utaelewa. Asante sana na karibu kujifunza pamoja.
ReplyDeleteAhsante kwa kushare. Mungu akubariki Sana.
ReplyDeleteMT RITA WA KASHIA anatemba miujiza mingi sana, mimi pia nimebarikiwa na miujiza yake. Ukiwa na shida yoyote haijalishi ina ukubwa gani omba kupitia maombezi ya MT RITA utajibiwa. Mbarikiwe watu wa Mungu
ReplyDeleteNanazidi kubarikiwa na Mt.Ritha Mtakatifu wa Mungu. Mnamo mwaka 2017 nilipata kukutana na kitabu cha Novena za Mt huyu katika kituo kimoja cha Hija jiji Dar Es Salaam. Ndipo nikaanza kusoma historia yake na nikajikuta navutiwa sana na maisha yake ya Imani katika magumu alivyokuwa akiyapitia. Kwa fundisho gumu na la kipekee kujifunza. MT.RITHA Alinishangaza kuomba hata kushiriki mateso aliyopata Yesu.
ReplyDeleteNi funzo gumu kwa binadamu wa kawaida. Nikiandika nia zangu nilimshirikisha mama huyu na nilikuwa nikikaa mbele ya Ekaristi kila mara asubuhi kabla ya kuanza kazi niliabudu kisha nitasali Novena hizi. Hivi ninavyoandika January 2019.Tayari ninavyoongea Maombi yangu manne makubwa kabisa yameshajibiwa..niliomba Mungu anipe Ardhi(Shamba) na pia Aniwezeshe mim na familia yangu Tuweze kumiliki nyumba, zaid niliomba kwa ajili ya binti yang ili apate kufaulu kuingia chuo Kikuu..Tayari sasa 2019 anasomea sheria mwaka wa kwanza.. Yote haya Mungu amekwishanitendea kupitia Mt.Ritha Wa Acacia.
Naamini kuwa; Hata yale ambayo hayajaonekana kutimia kwa macho naamini katika ulimwengu wa roho yamekushakuwako tayari.
Nawatkia moyo Wakristo usikate tamaa tusali bila kuchoka. Mt.Ritha wa Akacia uzuri kutuombea
.shukran za pekee kwa wote walioanzisha ukurasa huu..Mungu awabariki sana
Amina. Mungu atukuzwe na Utukufu ni kwake juu mbinguni
DeleteAmina,nami pia nimeokolewa sana na Mt.Rita mama huyu kupitia Novena yake.Hakika Mungu anatenda
DeleteNimepata ushuhuda kutoka kwa mtu aliyeomba kupitia huyu mama Na mm nmevutiwa sana kusali novena hii
ReplyDeleteAsante sana umenifungua Mno siwezi Kata tamaa tena!!
ReplyDeleteAsante kwa kuniimarisha katika imani hii kubwa. Nina shida nyingi na no dhaifu katika kukamilisha novena zangu kwa Mt Rita. Hats hivyo Nina imani kubwa maombi yangu yatatimizwa.
ReplyDeleteMm pia Mungu aliniona kupitia maombezi ya mtakatifu rita
ReplyDeleteNilifunga na kusali novena ya siku 9 ombi kuu likiwa ni kupata kazi maana nilijiajiri lakin wazaz wangu walipenda sana niajiriwe kwasababu ya elimu yangu
Cku ninayomaliza novena niliongea na mama mmoja kwamba akisikia popote kuna kazi bas aniambie
Akasema sawa
Bas cku nikaenda jumuia nikakutana na mume wa huyo mama akaniambia kesho njoo ofisini
Nkashtuka kwanza maana ckutarajia kama itakua haraka hivo maana huyo mume wake ana kampuni nyng tu hapa Tanzania na nje pia
Nilivoenda nikaulizwa nmesomea nn nkamwambia, bas nkakabidhiwa pale nikaambiwa j3 njoo uanze kazi😀😀
Aise sikuamini
Ckuapply popote, ckwenda na cv wala chochote yan nilifurahi
Hivi sasa mm ni manager wa usalama,afya na mazingira katika kampuni nne hapa dar
Hii novena naikubali sana
🙏🙏
Mimi nimeanza leo ila kwa imani kubwa atafanikiwa
DeleteUmenipa nguvu kwa kweli,,,kuna watu wawili wameshanidokeza kuhusiana na novena ya mt Rita,,wamenambia ukiomba kwa Mungu jambo lako lililoshindikana kupitia mt Rita utajibiwa haraka sana,,,ndo na mm natafuta kitabu
DeleteNimefalijika sana nilipo soma ujumbe huu mungu akubariki sana
ReplyDeleteHa uko vizuri dada hongera nimefarijika sna kwa ujumbe mzuri nimepata kitu
ReplyDeleteThanks a lot for sharing the massage with us #feeling blessed
ReplyDeleteTunamshukuru sana Mungu kwa ajili ya maisha ya mama huyu, hata mimi amekua msaada wangu mkubwa katika maombezi. Naamini ataendelea kutenda miujiza kwangu na kwa wengine wote ambao wanamuomba. Mtakatifu wa mambo yaliyoshindikana.Asante sana Mungu, Asante Yesu sifa kwa Yesu.QQq
ReplyDeleteEe mtakatifu Rita nitendee na mimi, Amina
ReplyDeleteComprehensive Neurological Care Victoria was established in 2013 by Dr. Raju Yerra. After being based in the area for over 10 years, Dr. Yerra saw an acute need for a comprehensive neurological service in these regions of Melbourne.
ReplyDeleteNeurologist Melbourne
Nimebarikiwa sana binafsi nimefanyiwa miujiza mingi kupitia maombezi ya huyu mama
ReplyDeleteMungu atukuzwe kwa ajili nguvu iliyo ndani ya novena ya mtakatifu rithsa
ReplyDelete