Napata kigugumizi kutoa tafsiri halisi ya hilo neno la kigeni lililochukua kichwa cha mafundisho yangu mafupi, lakini nina uhakika wa zaidi ya 95% kwamba unaelewa lina maana gani kwa upande wako. Kwa upande wangu naweza kusema ni ahadi waliyowekeana watu wawili au zaidi (mara nyingi ni kukutana) ili kupeana au kujadili kitu au jambo muhimu sana. Mara nyingi yule aliyeahidiwa kamoyo huwa kanamkereketa na kutamani kubashiri nini kitazungumzwa, napengine kujiambia ‘bila shaka atanipa bonge la surprise leo’ au ‘ mh, Mungu wangu, sijuwi kuna baya gani nimefanya, atanishushuaje leo?’ .Kama ni binti kapewa hiyo appointment na mvulana asiyempenda, tayari anaandaa makombora ya maneno ya kumrushia maana jamaa huenda anataka kufanya application, au kama huyu mtoa appointment anapendwa basi binti anajiandaa vyema kupokea application na pia anafanya screening ya maswali ya interview kwa huyu jamaa, yasije kuwa mengi yaka m-boa na kubadili mawazo.
Lengo langu sio kujadili aina za appointment, la hasha! Bali ‘HUWA UNAJIAANDAAJE KUHAKIKISHA UNATEKELEZA APPOINTMENT ULIYOWEKEWA NA MTU UNAYEMPENDA SANA?’ Kuna rafiki yangu alikuwa anapenda sana kulala. Ikifika saa nne usiku, yuko fofofo square kitandani, hakuna alarm wala mtu anaweza kumuamsha hadi saa 12 alfjiri. Siku moja aliambiwa na mtu fulani muhimu kwake. ‘Please saa 6 kamili usiku nitakupigia nikwambie jambo muhimu sana, out of that utajutia na tusilaumiane’. Mh patamu hapo. Jamaa aliwaza sana. Aliweka mikakati ya kutosha, aliweka alarm nyingi mno, tena akaweka maximum volume, na akaweka karibu na kichwa chake. Akawaambia na roommate wote, ikifika saa tano na dk 50 hajaamka, wammwagie hata maji ili mradi tu aamke asikilize ahadi aliyopewa. Kama kawaida saa 4 usiku akauchapa, chapiiiii. Heh, makubwa, saa 5 na nusu mtu kaamka mimacho kodoo, kaenda kuoga kabisa ili asisizie tena na sauti isije kukwaruza wakati wa mazungumzo, teh,teh, Nguki mie, kama hiyo haitoshi akawaambia wenzake waliokuwa wanasoma, ‘plz sitaki mikelele kuna mtu muhimu nitaongea naye soon’. Eh, sawa alarm zote zilikuwa zinaita akiwa kashaamka tayari. Saa sita ikafika, hakuna simu iliyoingia, mh, kuangalia kwenye simu hana salio, duh, kaomba simu kwa wenzake wakasema hawana salio, akaomba mwenzake amrushie mia tano ili aunge kifurushi, ile kurushiwa kumbe alikuwa na deni, kamiatano kakaishia juu kwa juu huko. Kha, alilia kwa hasira na uchungu, akaangalia saa yake au kachelewa kuamka, aku, alikuwa kawahi tu. Hakupata usingizi hadi asubuhi. Kwenye saa 12, simu ikapigwa na yule mdada, ile jamaa kupokea kwa hasira akaanza kulalama ‘we nyau why uliniweka that night mimi nahangaika usiku mzima haunipigii, chizi kabisa wewe, ehe, ulikuwa unaongea na nani?’ Binti akajibu kwa upole, ‘Nisamehe, saa nne ile mama alikuwa na tatizo nikampigia salio likaisha, nikategemea kuwa labda utanipigia wewe, uliposhindwa nikasema nitakupigia asubuhi nikwambie, lakini sasa naona umepokea kwa shari as if nilifanya makusudi, basi tena nakata simu na sitakuambia tena! Mh, kilichoendelea nitakuambia next time.
Umeona huyu jamaa fundi wa kulala alivyothamini appointment na kutumia mbinu zote kuhakikisha inatimia? Ehe vipi kwenye mambo ya kanisa mara ngapi tunapewa wito mbalimbali wa kutekeleza lakini visingizio kibao kuwa tumepitiwa na usingizi, mara tulikuwa busy, mara sio lazima kutekeleza mara kwa mara? Mara ngapi tumejitesa na kukosa usingizi ili kujibidiisha na mambo ya kanisa? Mara ngapi hata kusoma nakala na vitabu vya kanisa tunaona uvivu?. Kwenye appointment za kuleta raha za mwili tunakwenda hata kama kuna mvua ya kokoto, na tukifika huko hata tukiulizwa. ‘vipi umeumia?’ utasikia ‘Wala sijaumia, the way nakujali hata mvua sikuisikia, ilikuwa kama hali ya hewa nzuri ya kunipa nguvu ya kufika hapa kwako wewe nikupendaye!’ mh, sawa, Vipi mara ngapi Yesu wa Ekaristi anaweka appointment na sisi katika tabernacle , lakini tunazima simu na kutoa betri kabisa ili tusisikie alarm ya dhamiri yetu inapotuamsha. 2 Samuel 22:31 ‘Mungu njia yake ni kamilifu; Ahadi ya Bwana imehakikishwa; Yeye ndiye ngao yao Wote wanaomkimbilia.’ Sasa ahadi ya Kristu tunaipiga teke. Sijajua wewe mwenzangu unachukuliaje huku kuhakikishiwa kwa ahadi ya Bwana, maana mikono yake i wazi kutuambia jambo mhimu kwa manufaa yetu, sisi tunaotegemea wingi wa huruma zake. Vijana wa Kikristu tumke, tuweke maximum volume kwenye dhamiri zetu, ili tusikawie kukutana na Kristu.
Tumsifu Yesu Kristo,
Bsc Irrigation & Water Resources Engineering , SUA,2012-16
Eng Nguki Herman. M
Talking to TMCS SUA-New Hostels students. |
Talking to TMCS SUA-Main campus students. |
Talking to TMCS SUA-Main campus students. |
Kweli kaka Nguki appointment inatakiwa itimizwe kwa wakati,Tuwe waaminifu kwa Mungu tuirithi nchi na hatimaye peponi.Amina
ReplyDeletenice one
ReplyDelete