UKIMUA KUBADILIKA USIGEUKE TENA.
Washa mshumaa wa kujielewa, usifaanye ngono kabla na nje ya ndoa. |
Nimekutana na rafiki yangu kipenzi, kwa uchungu
akaniambia hili ambalo limempa ushujaa wa maamuzi. NAMNUKUU
‘ Nguki my friend, mwenzako wakati nipo O lever, sikuwa na mahusiano
mazuri sana na Mungu. Nilikuwa navutwa sana na tama za mwili. Nilikuwa na
mahusiano na msichana mmoja, japo hatukudumu sana, na baadaye msichana mwingine
ambaye huyu yeye alikuwa ananilazimisha yeye, na alinitongoza yeye na
nilishindwa kujizuia, tukafanya ngono kama ilivyo yule wa kwanza. Niliendelea
kuwatongoza wasichana wengine kama watatu hivi, japo kwa msaada wa Mungu
sikufanikiwa kufanya nao ngono. Nasema ni msaada wa Mungu kwakuwa mazingira
yalikuwa yananiruhusu kufanya uchafu huo na pesa kiasi cha kumudu uwezeshwaji
nilikuwa nayo.
Niliendelea na tabia ile kwa muda, na baadaye nikajifunza kuwa
nafanya ujinga na nitakufa endapo nitaendelea. Siku moja nilikaa na kujiuliza
hivi siwezi kujizuia? Hivi kwanini wasichana niliofanya nao ngono sijawajaza
mimba? Kwa nini sijaathirika na magonjwa? (baada ya kupima).. Nikajijibu
mwenyewe kuwa Mungu alikuwa kazini usiku na mchana kunitafuta nisipotee. Ili
kuthibitisha kuwa haya yanatoka moyoni
au la, sikumoja nikaingia kwenye mtego.
Kuna sehemu tulikutana wawili tu mimi
na Yule msichan ambaye hata sikumpenda ila alinitongoza na kunitengenezea mazingira ya kufanya ngono
naye hapo awali. Sasa hii ni awamu nyingine ambapo nimejiapia kubadilika,tena
tupo sehemu ya faragha kabisa. Mapigo ya moyo yalinienda mbio na sikutaka kurudi
uchafu ule. Hali ilizidi kuwa mbaya pale alipotoa nguo zake zote , moja baada
ya nyingine. Joto lilinipanda na kijasho chembamba kilianza kunitiririka
kikianzia mgongoni na hatimaye kwenye kwapa na maeneo mengine. Nikajiuliza hivi
Mungu wangu nataka kufanya nini hapa? Alinivuta ili nimkaribie. Lakini
nilikataa kwa nguvu na kubaki pale nilipokuwa nimekaa. Alinivuta tena mara
kadhaa, nikagoma huku nikimuomba Mungu anitoe salama katika midomo ile ya
shetani ambayo nimejipeleka mwenyewe. Huku akishindwa kuamini kinachotokea,
akijua labda natafuta momentum ya kumuendea, alianza kukasirika, na akaja kukaa
miguuni mwangu akiwa vile. Mapigo ya moyo sasa yaliacha kudunda kwa mfumo wa
nukta na kuhamia mfumo wa mstari nyoofu. HISIA ZILINIPANDA SANA KWAKUWA MIMI NI
MWANAUME NILIYE KAMILI, LAKINI NLIIBANA MIGUU YANGU VYEMA NA KUMWAMBIA MUNGU
SITAKI KUKOSEA LEO. Yule dada akaamini kuwa leo sio mimi wa siku zote. Kwa
hasira akasimama na kuvaa nguo zake na kuondoka. Nilishusha pumzi ndefu na
kukurupuka huku nikimshukuru Mungu. Na kuanzia siku ile nikaamini kuwa KUACHA
KABISA NGONO INAWEZEKANA hata kama ulizoea. MIAKA SABA BADAYE nimekutana na
mmoja wa wsichana niliyowahi kuwatongoza lakini sikufanya naye ngono, ambaye
pia anajua kuwa nimewahi kumtongoza na rafiki yake enzi hizo. Alinikuta nikiwa
mtulivu sana, huku nina Rozali yangu shingoni ambayo kipindi hicho nilikuwa
sivai. Walikuwa wawili na mwenzake, na watu wengi pia walikuwepo na shughuli
zao. Sikustaajabu kukutana naye, but akasema kwa nguvu ‘FULANIIIIII,
NAKUONA, ZA MIAKA MINGI? NAONA ROZALI NYINGI KAMA PASTOR VILE, KUMBE WIZI
MTUPU’. Maneno yale yalinichoma sana hasa ukizingatia ni mbele za watu. Kwa
ujasiri nikasema ‘ASANTE SANA NASHUKURU’ .Yeye alidhani anaonge na yule
wa miaka saba iliyopita, lakini kumbe nilibadilika totally na kuwa mtu mwingine
kabisa,najiheshimu na kumtegemea Mungu, tena nimefanikiwa katika nyanja
mbalimbali nayeye anahangaika tu, kwa
maana hata shule ilimshinda akaishia form four. Lakini sikujutia kwakuwa alijua
niliendelea na tabia ile.’ MWISHO WA KUNUKUU.
Nilimtia moyo na kumwambia
UKIAMUA KUBADILIKA, BASI USIGEUKE TENA , nikapongez ujasiri wake wa kunieleza
mambo ya ndani kabisa haya,. Ukiacha njia mbaya wapo watu watakao sema unaigza,
na wengine kukushawishi urudi ulikokuwa. Kaza mwendo, ngono inachakaza, ngono
inapoteza rasilimali hasa fedha na muda.
Ngono inakufanya usione umhimu wa kuifikia ndoa takatifu,ngono inavuruga
mahusiano yetu na Mungu, ngono inakufanya uwe wakala kamili wa shetani
kuishabikia zinaa,ngono inakufanya uishi kwa wasiwasi muda wote, ngono
inakufanya uone kila aliye mbele yako anafanya kama wewe , kumbe masikini uko
peke yako mahali hapo. Inawezekana. Kama jana hujafanya, leo pia na kesho
hufanyi, basi unauwezo na keshokutwa na wiki, mwezi ,mwaka hadi siku ya ndoa
kufurahia tendo la ndoa. Ufanyishe mazoezi ya kujitawala, na Mungu atakupa
nguvu zaidi. Tumsifu Yesu Kristu……………………….
Eng Nguki Herman. M
Asante kaka ujumbe mzuri
ReplyDeleteNashukuru, tuko pamoja, asante kwa kutembelea blog hii. Na endelea kufurahia mada mbalimbali za kukujenga.
Delete