‘Hellow Herman rafiki yangu mzima? Habari za siku nyingi?.
Aisee nilitaka kukwambia kuwa mwenzako wameukata na mguu wangu wa pili, kwahiyo
sahizi sina miguu yote, namshukuru Mungu kwa uzima, Bado nipo Ifakara huku, vipi
wewe huko, ndugu zetu wa SUA wanasemaje? Nawatakia masomo mema, na Mungu
awabariki sana ndugu zetu’ Ni maneno yaliyofanya nisimame na
kutetemeka kwa muda baada ya kuipokea simu iliyopigwa na rafiki yangu John,.
Yeye ni mlemavu wa ngozi (Albino) pia alikuwa amekatwa mguu mmoja kutokana na
ugonjwa wa kansa, pia mguu wa pili ulikuwa unamsumbua hivyo hata kutembea na
magongo ilikuwa ni kwa shida. Nilifahamiana naye katika kituo cha kulelea wazee
na wasiojiweza cha Fungafunga, manispaa ya Morogoro na kubadilishana namba za simu, ambapo ulikuwa
ni wajibu wetu wanajumuiya wa Sant’ Egidio na TMCS
kwenda kuwafariji na kuwahudumia tunapoweza. Hata wenzetu wa CCT, SDA,
hata vikundi vya madarasa walienda mara kadhaa kuwafariji na kuwahudumia.
Rafiki yangu huyu baada ya kuondoka Fungafunga alienda kuishi
Ifakara ambako hali ya mguu uliosalia ilizidi kuwa mbaya na hatimye kulazimika
kukatwa pia. Ajabu
ni kwamba wakati ananipigia alisikika akiongea kwa furaha na amani bila
wasiwasi wowote. Hakika nilijifunza kitu kupitia hali ile, kwa maana
ningetegemea angeongea kwa huzuni na kukata tama kwa maana hali aliyonayo ni
tete na yenye kuhitaji msaada zaidi. Lakini alimshukuru Mungu kwa uzima, tena
akatumia nafasi hiyo kunijulia hali mimi niliyekuwa mzima wa afya chuoni na
kunitakia masomo mema.
Kwa lugha rahisi ‘kila
mtu anauwezo wa kumsaidia kila mtu’. Makundi ya wahitaji yako mengi sana,
kuanzia hapo ulipo, kwa bahati mbaya huwa tunajikita kuangalia mahitaji ya vitu
vya kushikika (tangible things) kumbe wahitaji wengi wanataka faraja yetu,
wanahitaji kupewa tumaini kuwa wanapendwa na Mungu na pia uzima wao ni furaha
yetu sote. Kuwa na fedha nyingi sio kiashiria cha kuwa na furaha, la hasha,
zipo familia tajiri wa kila kitu, lakini wakiingia ndani baba na mama kila mtu
analala chumba chake. Sasa unajiuliza nini sababu? Mmoja huwa anakoroma sana na
kumkosesha usingizi mwenzake, au mmoja huwa analala ovyo kitanda hakitoshi
nakadharikaa, ni kwamba watu hawa wameunganishwa na vitu na sio upendo.
Mimi na wewe hasa vijana, tumshukuru Mungu kwa uzima, halafu
tupige hatua, tutoke nje kuona wahitaji, Papa Francis anasema ‘Muda wa kukaa na kujifungia ndani haupo,
uwe kasisi, uwe mtawa uwe mlei, toka nje uone kanisa linavyoteseka, toa msaada’
. Hata Mtakatifu Mama Teresa alipigilia msumari karama hii kwa kusema ‘Kama huwezi kuwahudumia watu mia moja,
basi hudumia mmoja’. Kila mtu ana kitu cha kitofauti cha kuweza kuwasaidia
wengine. Huna pesa, sawa, vipi hata kutabasamu
tu kwa mgonjwa unashindwa? Hata kushauri tu pale ambapo watoto wanakosea
unashindwa? Hata kusali tu kwaajili ya watu wasio na msaada nalo ni tatizo,
hata kushika mashavu tu ya watoto wadogo na kuwaombea afya njema nalo ni
tatizo? Mimi ni mlei na mwanandoa wa baadye, lakini kuwa katika utume wa
Sant’ Egidio imekuwa kama kuwa katika malezi ya seminari ambapo unajengeka kuwa
na macho ya kuona mahitaji ya makundi mengi zaidi na kuyabeba na kuwa kama
yako. Wpo waliojitesa ili wewe ufike hapo, hebu jibane basi hata kidogo ili
kuwapa ahueni ya maisha na wengine. ANZA LEO, INAWEZEKANA
VIVA SANT’
EGIDIO
Eng Nguki
wa Malekela- ngukiherman@ymail.com
Tabasamu la wahitaji ni ishara ya upendo wa Mungu.- |
during Christmas Lunch 2015- SUA |
Tukacheza na kuimba pamoja- Christmas Lunch SUA 2015 |
Tukala na kuwagawia zawadi-Christmas Lunch 2015-sua |
After Sunday Mass, Pamoja na Fr Aloyce na mafrateli wa Fransalian-SUA-2015 |
After mass, Pamoja na Fr Aloyce & my fellow Altar ministrant Carist Mwacha 2015-sua |
Bofya ‘view
the web version’ hapo chini ili uende main window na kujipakulia mada motomoto
kutoka kwa Nguki na ujifunze mengi. COMMENT AND SHARE.
The best moment ever.
ReplyDeleteGod bless you brother..
ReplyDeleteYou inspire me alot..
Thank you bro Zeno,we are together, we are one!!
DeleteAsante kaka kwa ujumbe mzuri mungu azidi kukupa nguvu katika utume wako
ReplyDeleteAmina, asante pia. Tuko pamoja my mwenyekiti Elius
ReplyDelete