KAZI YAKO NI
KUOGELEA, USIKUBALI KUUZIWA HELMET YA TOPE/UDONGO
USIPOTEZE MUDA KWA KUWEKEZA KWENYE NGONO, WEKEZA KWENYE MAISHA, MSHUMAA WAKO WA MAISHA USIKUBALI KUUZIMISHA KIRAHISI |
Habari yako ndugu, Nguki
nakusalimu, najua kichwa chako chamotoooo kwa habari za Scorpion mtoboa
macho na sarakasi za walimu wa field
Mbeya day. Inawezekana kabisa mimi na wewe tuna madudu yetu tunayafanya kwa
siri na Mungu anatuepusha tu na mchukua video, maana tukinaswa na kufanikiwa
kuingia watsup, basi nina uhakika aibu tutakayopata ni yakiwango cha lami, bila
shaka itatulaza na viatu kwa fedheha. Hivyo tujifunze kupitia makosa yawengine kwa maana ndiyo sifa ya mtu
mwerevu, lakini kwa mjinga haamini hadi
ya mkute yeye ili wengine wajifunzie kwake.
Naam. Katika pitapita zangu huku kwetu aridhi ya Mkwawa nikakuta kijana
mmoja wa kiume amevaa vizuri na kapendeza sana. Kiufupi nilimfurahia kwa uvaaji
wake. Baada ya sekunde kadhaa akatokea binti mmoja na kuanza kumfutafuta
kichwani kanakwamba jamaa anavumbi, japo alikuwa msafi. Binti mwingine alikuwa
pembeni akamwambia ‘Unazingua wewe, mfute na viatu basi’ Yule dada kweli kwa
mikono yake akaanza kumfuta viatu yule kaka ambavyo vilikuwa na vumbi.
Sikushangaa kwa maana mambo haya ni kawaida mjini na vijijini na yule dada
hakujali watu wanaoshangaa pale. Moyoni mwangu nikajiwazia, ‘ lazima kuna kitu kimemscorpion huyu dada na
kujitoa ufahamu’. Kaka mmoja akasikika akisema ‘Duh, huyu mshikaji noma,
yani akipata hela , dada zetu wa hapa utulivu huwa unapotea kabisa, anawachezea
anapotaka, yani utadhani ataishi milele, ni aibu sana, tana familia yao
inauwezo sana kifedha, bora tu angeoa na kutulia, kama ni magonjwa basi
atasambaza vya kutosha, kama unavyoona fulani pale (akamtaaja jina) anatamani
hadi kumlamba miguu huyu jamaa, kisa hela. Hatari sana’. Ahaa, kumbeeeee,
nimeshakipata kilichomtoboa macho ya utashi na kujifanya chizi, ndio ni FEDHA
ZA WATU AMBAZO HAZITOLEI JASHO KUZIPATA. Maisha ya kijana ni yakupambana, maisha
ya kijana ni ya kuwaza mbali na kujitabiria mazuri na makubwa. Lakini aina ya
uwekezaji wetu unakatisha tamaa, tumewekeza kwenye vitu vya aibu, vitu ambavyo
hatuwezi kujisifia mbele za kadamnasi kuwa tunafanya. Sijuwi kama unanielewa.
Kama kweli unajiwazia mazuri wewe na wenzako, huwezi kutumia fedha zako
kuwekeza kwenye ngono, ni ujinga huo, the same kwa msichana mwenye akili hawezi
utumia mwili wake kama ulimbo wa kuvuta wafanya ngono. Huo ni utamaduni wa
kilevi na nimeufananisha na mtu anayenunuua helmet ya udongo wakati kazi yake
ni kuogelea, bila shaka mara atakapogusa maji tu, italowana na kubomoka hivyo
kuchafua maji na pia uchafu utamuingia machoni hivyo kutoona mbali ‘having limited spectrum’. Tamani kila
mtu akutabirie mema kwa maana wewe sio muharibifu wa maisha ya watu. Ishi
maisha ya kusaidia wenzako, sio tu kifedha, hata mawazo na kumsihi Mungu awatoe
katika mateso wanayopitia ili nao waone kuna umuhimu wa kuishi. USIKUBALI KUUZIWA HELMET YA UDONGO WAKATI
KAZI YAKO NI KUOGELEA . ………………
Eng Nguki Herman. M
Wadada jamani mwanaume sio mtaji! Tujifunze kuwa na nidhamu na pia tujiheshimu! Hongera Hermani. Naamini wengi watapona kupitia blog yako
ReplyDeleteThank you Glory. We are together
ReplyDeleteKweli kaka asante kutuelimisha na kutukumbusha kwa hili vijana tunajisahau sana, Mungu azidi kukutianguvu.
ReplyDelete