USIONE AIBU, WEWE NI SHUJAA
WA UHAI, MTETEZI WA MAISHA.
Usidhaani kafumba macho, anakuona sana. Sema anawaza lini atakuwa kama wewe |
Soma taratibu………………….
Duh, aisee, kweli usijihesabie kuwa una duka eti kwasababu upo kwenye gari kwenda kununua vitu. Mama J anasimulia :
Kaka Nguki we acha tu ndugu yangu, yani hii dunia usikutane na mtu anacheka barabarani huko, ukadhani mambo yake ni mazuri tangu kuzaliwa kwake. Mwaka juzi nilibahatika kupata mchumba ambaye alikuwa ananipenda sana, na nilimshukuru zaidi Mungu kwa maana tulipoweka mezani suala la kutofanya ngono hadi tufunge ndoa, wote tulilipokea vizuri, alikuwa ananihudumia kwa mambo madogo madogo huku tukizidi kufahamiana tabia na vitu kama hivyo. Mwaka jana mwezi wa nane baba yangu alikuwa anaumwa sana kijijini huko wilaya ya Ifunda. Si unajua mimi naishi hapa Iringa mjini na nimepanga chumba mimi na rafiki yangu na tunafanya kazi zetu ndogondogo za ujasiliamali. Basi hiyo mwaka jana mwezi wa nane nikaamua kwenda kumuona baba yangu ambaye alikuwa anaumwa sana na anauguzwa na mama yangu mzazi. Kule kwetu gari linaenda moja tu na linatokea Mafinga, ukilikosa hilo basi. Nilifanikiwa kwenda hadi kule, nikawapa pole kwa mgonjwa, pia nikamwambia mama kuhusu huyu mchumba wangu ambaye yupo tayari muda wowote kuanzia sasa kuja kutoa kila kitu huku, na mimi nifunge ndoa mama, heheeeeee, (tulicheka na kugongesha viganja vya mikono yetu mimi na mama). Basi baada ya siku kadhaa, niliaga ili nirudi nyumbani. Bhati nzuri jirani yetu kuna baba mmoja ana gari na alikuwa na safari ya kwenda Mafinga, na aliposikia nasubiri gari la kwenda huko alishauri nipate lift kwenye gari lake. Nikashukuru na kufurahi maana nauli imepona hapa.
Safari ikaanza, kwenye gari lake tulikuwa na vijana wengine watatu, jumla watano. Basi wakati safari inaendelea kumbe wale vijana walikuwa hawafiki Mafinga, walishuka njiani mmoja baada ya mwingine vijiji vya njiani na nikabaki mimi na Yule baba mwenye gari, safari ikaendelea. Tulipofika katikati ya msitu alianza kunitazama kwa kunitamani na kuniongelesha maneno ya kunitaka. Nilianza kupata hofu na kutetemeka, nikajua anatania, nilimjibu kuwa sitaki na ninamuheshimu kwa kuwa ana mke na watoto. Alijifanya hasikii na kuendelea kunisemesha, nikaomba kushuka kwenye gari, akakataa. BAADA YA MUDA AKASIMAMISHA GARI PEMBEZONI MWA BARABARA, KUANZA KUNISHIKA, NILILIA SANA HUKU NIKIWAZA MADHARA YAKE PAMOJA NA HATIMA YANGU NA MCHUMBA WANGU MTARAJIWA. NILIPIGA KELELE, NA SIKUPATA MSAADA, NA AKAFANIKIWA KUFANYA UCHAFU WAKE PASIPO RIDHAA YANGU. Akaendelea uendesha gari hadi mafinga na kunishusha hapo. Niliahirisha safari ya kwenda Iringa mjini ambapo kesho yake nilipaanda tena gari kurudi kijijini kwa mama kumwambia yaliyonikuta. MAMA ALILAANI SANA KITEND HIKI CHA KITATILI. PIA AKASEMA NIFANYE MCHAKATO WA KUPIMA, NA ANAMUOMA SANA MUNGU AWE HAJANIAMBUKIZA MAGONJWA, LAKINI KAMA AKIWA KANIPA MIMBA, NI BORA NIKAITOE ILI NISIMKOSE MCHUMBA WANGU KULE IRINGA MJINI. MAMA ALISISITIZA NISIKUBALI KUBEBA MIMBA AMBAYO NI ZAO LA UBAKAJI NIKIIKUTA, NITOE HARAKA SANA. Basi nikapanda tena basi kesho yake hadi mafinga na kupanda jingine hadi Iringa mjini. Nilikaa siku chache na kwenda kupimwa, Mungu wangu, NILIKUTWA NINA MIMBA! Kha, jamani masikini mimi,yani mra mmoja tu!! nililia sana. Lakini sikukutwa na ugonjwa mwingine.Ushauri wa mama ukaanza kunijia, lakini nikasema SITAMUUA MTOTO ASIYE NA KOSA, NITAKAA KIMYA NA MAMA NITAMWAMBIA TUMBO LIKIWA KUBWA AMBAPO USHARI WA KUTOA UTAMAANISHA KUNIUA MIMI PIA MCHANA KWEUPE!! Niliwaza kumficha mpenzi wangu Yule, lakini nikaona moyo unaniuma sana, na usafi wa moyo niliomuahidi Mungu nay eye ,haupo tena. Nikajiwazia liwalo na liwe, NINAMWAMBIA UKWELI. Nikamuita nyumbani yule mchumba wangu mtarajiwa, huku nikivuja chozi lililochanganikana na jasho jingi nilimueleza kila kitu, na kumpa uhuru kama ataendelea na mimi sawa, kama ataniacha sawa. NIPO TAYARI KWA YOTE. Yule mkaka alisikitika sana, japo hakunilalamikia, hakunitukana, wala kunlaumu. Lakini alinipa pole na kuuondoa mguu wake moja kwa moja, na hakurudi tena, iakawa ndio kuachwa kwenyewe. Nilianza kuishi kwa shida, lakini rafiki niliyekuwa naishi naye alikuwa ananifariji na kunitia moyo sana na kwamba nipige moyo konde na Mungu mtoa vyote ataleta tumaini badaye na mateso haya yana siri ndani yake. Nilitafuta namba ya yule mbaba aliyenibaka na kunipa mimba, kila nikimpigia, alikuwa akinitukana na kunikatia simu, nilikuwa naumia sana, lakini sikuwa na jinsi nyingine.
Mimba ilivyokuwa kuwa kubwa nilimtaarifu mama. Alisikitika sana,lakini wazo lake la kuitoa lilikuwa limechelewa. Hakuwa na la kusema. Mwezi wa sita mwaka huu nikajifungua mtoto wa kike kwa msaada wa mama mzazi wa huyu rafiki yangu (Ndio huyu J unayemuona) anamiezi mine sahizi. Namshukuru Mungu kwa huli jaribu kubwa lililotaka kunitoa uhai wangu. Baada ya kusikia nimejifungua motto, Yule aliyenipa mimba mara mojamoja huwa ananipigia simu kuulizia hali, nakasirika sana na ananikumbusha machungu muuaji yule.Namuachia Mungu yote. @@@@@@@@@@@@@@@ Nguki baada ya pumzi ndefuuuuuu, nikamshika J , mwenye miezi mine, katoto kazuri, kerembo, kanavutia, kamebeba siri ya Mungu. Niliongea mengiiiiiiii ya kumpa nguvu, na kwamba Mungu atampa mume bora kabisa ambaye atawapenda yeye na J wake. Kuwa na mtoto huyo hakuna maana yeye ni mdhambi, wala asimchukie mtoto huyo, huyo huenda akawa ni tumaini na msaada mkubwa kwa watu wengi. Kristu ni mzima, wanaume tuache tama za mfumo huu, huu ni uuaji, uwe umeoa au hujaoa, tawala nafsi yako, wekeza kwenye sala. Ukiwa na tabia za aina hii wewe hauna utofauti na mchawi kwa maana kazi yako ni kutengeneza matatizo kwa wangonge.
BADILIKAAAAAAAAAAAAAA Tafakari Njema…..
Eng Nguki Herman. M
Bofya view the web version chini ya document ikupeleke main window, ujipakulie mada nyingine motomoto. Comment and SHARE
Washa mshumaa wa mawazo chanya. Kuwa mtetezi wa uhai, acha ukatili |
Hasimwambie akikua
ReplyDelete