Kutabasamu na kufurahi ni dawa kwako na kwa wanaokuzunguka. Smile, laugh ,,,, mama. |
Kuna wakaati mada hii huwa napenda kuipa jina WEATHER STATION. Bila shaka unafahamu maana ya weather station au kituo cha hali ya hewa kwa Kiswahili. Kazi yake ni kukusanya takwimu zilizopo za hali ya hewa ili kubshiri matukio ya kihali ya hewa yatakayotokea huko mbeleni. Lakini hawa jamaa wanaofnya kazi kwenye hivi vituo au mamlaka wana rah asana, kwa maana ikitokea walichobashiri hakijatokea, maelezo yao ni marahisi tu, utasikia, ‘kulitokea mgandamizo wa hewa wapi huko ukasababisha upepo ubadili muelekeo badala ya kuvuma kwa 25km/hr kwenda Multpurpose hall, ukavuma kwa 200 km/hr kwenda freedom square Mazimbu. Na tena ikitokea walichobashiri mmepuuzia na kikatokea, pia neno lao fupi tu, ‘tuliwaambia mkabisha’ . Kwa kifupi muda wote wapo sahihi.
Tabia ya binadamu kuna wakati inafanana na weather parameters kama temperature, humidity na ndugu zao, japo kamwe haiwezi kujengewa weather station ili ku predict trend ya ubadilikaji na kuchora graph zake. Kwa maana hiyo, kamwe huwezi kubashiri kwamba kwa maneno haya, huyu atayaishi anayozungumza au la! Siku mgandamizo ukizidi kaskazini atatoa majibu rahisi ya badiliko lake, wakati wewe ulishamchorea graph tena kwa peni, hata kifutio hakina kazi. Kuna wakati watoto wanabadilika hata kwa wazazi wao walio wazaa, fikiria graph iliyochorwa na mzazi hasa mama aliyekulea kuanzia tumboni miezi 9 na wengine miezi 12 sijuwi, sembuse kwa wewe mliyekutana tu hapa au pale? Mh, sasa kumbe ni bora kujijengea indoor self-weather station ya kujichunguza wewe binafsi na kujichorea migraph yako mwenyewe ili hata ukipredict upepo, lakini ikaja mvua ya kokoto, au ulipredict manyunyu ya mvua, lakini likaja tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 20 kipimo cha lichter ikuhusu mwenyewe. Kuna siri kubwa moja tu, ya kuhakikishaa muda mwingi unakuwa una furaha na graph zako zinakaa vizuri.
- Mithali 15:13 Moyo wa furaha huchangamsha uso; Bali kwa huzuni ya moyo roho hupondeka.
- Joel 1:12 Mzabibu umesinyaa, mtini nao umevia; Nao mkomamanga na mtende na mtofaa; Naam, miti yote ya mashamba imekauka; Maana furaha imekauka katika wanadamu.
- 2Corinthians 7:4 Ninao ujasiri mwingi kwenu; naona fahari kuu juu yenu. Nimejaa faraja, katika dhiki yetu yote nimejaa furaha ya kupita kiasi.
SIRI NI KUWA MCHESHI (SENSE OF HUMOUR) KWA KILA AWAYE MBELE YAKO HUKU UKISALI NA KUMTEGEMEA MUNGU KWA KILA KITU.
Kwanini uwe mcheshi?
1. It Attracts People To You. Watu wanapenda kukutana na nyuso zenye furaha, kufurahi ni dawa hasa pale ambapo mmoja anakuwa na msongo wa mawazo kwa namna moja au nyingine. Kucheka ni tiba kwa mtu aliyekosa tumaini na hatia ya kukataaliwa.
2. It Attracts The Right Kinds Of People. Mtu mcheshi Mungu humkutanisha na watu sahihi. Ukijifanya fundi wa kujinunisha na shetani atawanunilize watakaokujia ili chuma inoe chuma. Kujifanya wewe ni watofautisana kuliko wenzako sio tabia nzuri.
3. Cope With Stress. Mtu mcheshi yuko frexible, hata anapopata magumu ucheshi wake humsitiri. “A person without a sense of humor is like a wagon without springs. “A person without a sense of humor is like a wagon without springs. It's jolted by every pebble on the road. “ Henry Ward Beecher.
4. Health Benefits. Laughing has been shown to improve your immune system by helping your body produce more infection fighting materials and lower the amount of stress hormones in your body.
Furaha ikitoka moyoni, uso hauna uwezo wa kuficha ujue, teh,teh. With my young sister ,,,Damiana |
5. Humor Improves Your Mood. Mtu mcheshi mood yake iko vizuri katika utendaji kazi, tena hakwziki mara kwa mara na akikwazika anasamehe mara moja, pia akimkwaza mtu yupo huru kuomba msamaha.
6. It's Good For Your Brain.Utafiti unaonesha utani mpya na kucheka huamsha sehemu ya ubongo ambayo ni muhimu kwa kujifunzia na kutafakari.( University of London of Neurology). “Humor is by far the most significant activity of the human brain.”• Edward de Bono.• Edward de Bono. Huo ni ukweli wa mchana. Kama huamini fuatilia mtu aliye na stress na hasira, halafu apewe kazi ya group kutype, msiruhusu akaiprint, pitieni kwanza pamoja nayeye akitlia. Mtajionea vituko, kwenye O ataweka sifuri, problem kaandika bloplem etc,,,,
7. It Strengthens Friendships. People feel closer to others who they are able to have a good laugh with. By joking around with friends and family you are not only enjoy a good time with someone you care about, you are also building a bond and a memory that you guys will be able to come back to later on. We jinunishe tu, watu watakuwa hawaji kwako mara kwa mara kukushauri au kushare na wewe chochote.
8. Diffuse Anger. Mtu mcheshi hufanya watu wasiwe na hasira juu yake hata akifanya kosa (kwa bahati mbaya), ni rahisi kusamehewa. Ni afya kujishusha hasira zako, na kushusha za wengine pia. " You can't stay mad at someone who makes you laugh- it's as simple ast that."- Jay Leno.
9. Lowers Other People's Resistance. Kama binadamu, tuna ugumu/ resistance kwa mambo fulani fulani. Kwa mfano kuintroduce jambo fulani muhimu kwa mara ya kwanza kwa mtu fulani. Mtu mcheshi anafanya iwe rahisi watu kumshirikisha au kumwambia mambo mengi. Eg kupropose urafiki/uchumba etc. By using humor and being funny you can break through these lines of resistance, or at least lower them, so that you can meet new people, ask important questions, or whatever you want to get done. Humor is a rubber sword - it allows you to make a point without drawing blood. ~Mary Hirsch.
10. Help Those Around You. Kuwa mcheshi kunafanya uwasaidie wanaokuzunguka na kutatua matatizo yao. Knowing that you are making someone else's day and you are helping them relax and enjoy life for a minute can be rewarding all by itself. The friendships you can build are just a nice added bonus to that. Kufurahi na kuwa mcheshi ni dawa ya kuboresha maisha yako, tena kutakufanya uishi kwa amani hata kama kuna ugumu fulani unapitia. Furahi,furahi,furahi.
Ukiwa mtu wa tabasamu na furaha muda mwingi, utakuwa na marafiki wa kweli. |
Nakutakia ujenzi mwema wa INDOOR SELF WEATHER STATION’ na Mungu atakusimamia.
TUMSIFU YESU KRISTO.
Eng Nguki Herman. M
Email: ngukiherman@ymail.com
Instagram: @eng.ngukiwamalekela
Twitter: @engngukiherman
www.ngukiherman.blogspot.com
click home/view the web version down the page to see other topics list (incase you don't) |
No comments:
Post a Comment