RAHA, KARAHA??? TUSIWAUMIZE.
Kwanini asinenepe kwa mfano? Hapo atajifungua salama mtoto mwenye afya. |
Katika mizunguko yangu ya siku zote, huyooooooo hadi
hospitali ya mkoa wa Njombe maarufu kama
Kibena. Wakati nimekaa nje ya hospitali kando ya barabara nikamuona mama mmoja
(sio mkubwa sana, ni binti kijana) ambaye alikuwa mjamzito. Alikaa chini kabisa
kwenye nyasi huku akiwa mpole na akionekna kutafkari na mwenye mawazo mengi
sana. Kiufupi ilionekana kuna kitu kinamuumiza kichwani kwake, au anamaumivu ya
mwili, si unajua tena hawa ndugu zetu wakiwa katika hali hiyo complications
kibao.
Baada ya muda mfupi watu wakatokea hospitalini kuja upande wa
barabarani. Ni kijana mmoja na binti mmoja ambaye alikuwa mjamzito pia. Bila
shaka walikuwa mtu na mkewe kwa maana niliona Yule mkaka kamshikia mkoba huyu
dada, pia kamshika mkono huku wakiwa wanatazamana usoni kwa bashasha na
matabasamu ya kukata na shoka. Kha, nikajua ni mimi tu ndio nilikuwa nawangalia
wale watu kama sehemu ya tuition, kumbe hata yule dada aliyekaa kinyonge pale
chini alikuwa anawakodolea macho vizuri tu. Muonekano wa wawili hawa ulitoa
picha ya moja kwa moja kuwa wanaishi maisha ya furaha na walijipanga vya
kutosha, tena hawajutii maamuzi yao na matokeo yake. Yule dada pale chini
liendelea kuwaangalia kwa uchungu huku machozi yakimlengalenga (sina hakika
kama ni Kiswahili sahihi), aliwangalia hadi walipovuka barabara na kuendelea
kuwasindikiza kwa macho hadi walipoingia kwenye gari la kuelekea Njombe mjini.
Kisha akajiinamia chini huku ameshika shavu lake.
Mimi kama kijana nilijiuliza maswali mengi mepesimepesi na
kujijibu mwenyewe. Kwa mfano huyu mama hapa chini tena akiwa kachafuka na vumbi
huenda kaolewa lakini mumewe hajuwi majukumu yake kwa matokeo ya kile ambacho
alikifanya yeye mwenyewe. Au yamkini akawa hii mimba kapewa na mtu ambaye
hajamuoa bado hivyo mhusika kakataa kushughulikia lolote nakadhalika, au
pengine jamii nzima inayomzunguka imemtenga kwa mfumo fulani.
Ndugu zangu mama mjamzito mwenye msongo wa mawazo sio tu huathiri mfumo wa kawaida wa maisha
yake, lakini pia huathiri afya ya mtoto tumboni nap engine kumzaa motto mwenye
afya mbovu ya mwili au akili au vyote kwa pamoja. Mvulana ukikurupuka kwa
kuendeshwa na hashiki za mwili kasha kumdandia kwa pupa huyo uliyemshawishi kwa
pesa zako, unatengeneza bomu ambalo litakulpukia hapahapa duniani au hata ile
siku utakaporudi kwa yule aliyekuleta duniani.
Mfano hebu fikiria mama mjamzito ambaye kaolewa na yuko na
mumewe nymbani halafu usiku tumbo limuume kidogo, utasikia:
Mama : We baba kijacho, amka bhana mwanao kanipiga teke
tumboni hapa, linauma sana.
Baba : Oh, pole my
love, kwahiyo ngoja nimpigie rafiki yangu aje na tax twende hospitali.
Mama : Hapana acha tu
usiku sahizi, nitajitahidi kuvumilia tutaenda hata asubuhi.
Baba : Hapana, plz,
au tumpigie simu Dakitari aje akucheck hapahapa nyumbani.
Mama : Mhhh, usiku
wote huu, usijisumbue, acha tu mume wangu.
Baba : Haya mama,
basi ngoja tukae wote, silali hadi muanze
kulala wewe na kijacho wangu.
Mama : Hahaaa, acha
bhana, unadhani tumbo lenyewe linauma sana basi, nilitaka tu uamke nikusikie
kidogo baba kijacho waangu.
Baba : Duh, jamani haya mama. Minahamu na huyo
kijacho kama nini, sijui katakuwa kajogoo,au mama ndio atajipatia mke
mwenza,, teh, heh, (anacheka huku akimbusu tumboni mkewe). Akizaliwa
nitamwambia ulimsingizia kuwa kakupiga teke kwa ndani kumbe ulitaka kusikia tu
sauti ya baba yake. Haya mama, lala basi nikufunike shuka. … …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………
Umeona haya majadiliano? YANA AFYA, RAHA nakadharika.
Hebu tuwe wakweli. Dada ambaye kapewa mimba na mtu ambaye
hajamuoa bado. Hapo nyumbani wamemdongoa hadi basi, wamemsondea dole hadi basi,
(hadi huyo motto anajiuliza kwani huko nje kuna vita?) tumbo likiuma usiku
anamuamsha nani? HAKUNA KITU ZAIDI YA KUJIONA MKOSAJI NA KUMCHUKIA MTOTO ANGALI
YUKO TUMBONI. Kwa bahati mbaya mtu ambaye hayajamkuta, anaona ni kitu cha
kufikirika nay eye hakiwezi kumkuta wakati hataki kubadilika. Huo ni mtazamo wa
mtu mjinga.
Soon tutakuwa wawili, teh,teh, karibu sana mgeni, kama nakusikia hivi kwa mbaliii |
Maana mwerevu hujifunza kupitia matatizo ya watu wengine, lakini
mjinga haamini hadi yamkute yeye, ili werevu wajifunzie kwake kama sample
space.
Badilika na uchukue hatua leo, kama ulishakosea basi usirudie
tena, na kama Mungu amekuepusha hadi sasa, basi usifanye makosa kwenye kufanya
maamuzi. Fanya uchaguzi sahihi, funga ndoa halali, furahia wakati wa ujauzito
wako/ wa mkeo kwa raha zenu. Inawezekana…………….Tafakari njema
Upendo uwake usiku na mchana katika familia zetu. Lakini wakati wa ujauzito mwanamke anatakiwa kuoneshwa upendo mara dufu zaidi kuliko kawaida kwa maana anaujumbe wa Mungu tumboni mwake. |
Watoto ni malaika. Wapewe haki ya kuishi tangu siku ya kutungwa mimba yao na kuendelea. |
Eng Nguki Herman. M
Email: ngukiherman@ymail.com
Instagram: @eng.ngukiwamalekela
Twitter: @engngukiherman
UCE Tanzania Volunteer
ngukiherman.blogspot.com / ucetanzania.org
click home to see the main page and other topics
click home to see the main page and other topics
Wakaka nasi tufikiri kwa makini sio lawama kuwapa wadada tu,kwani mimba walikunywa kwenye maji? basi tubadilike wote .Kaka Nguki elimu unayotupa sijui wanaelewa wangapi,duuuuh! God be with you all the lifetime
ReplyDeleteThanks indeed Cletus. Mungu atusaidie sana kaka tupate kuelewa haya.
ReplyDelete